MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Jaffo Aagiza Kufufuliwa Vilivyokuwa Viwanda Vya Serikali
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Jaffo Aagiza Kufufuliwa Vilivyokuwa Viwanda Vya Serikali
Habari

Jaffo Aagiza Kufufuliwa Vilivyokuwa Viwanda Vya Serikali

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Seleman Jaffo amewaagiza wanaomiliki viwanda ambavyo vilikuwa mali ya Serikali, vikafa kuhakikisha wanavifufua kabla ya kulazimishwa na Serikali.
Jaffo ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari alipotoa taarifa ya maendeleo ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dodoma.
Amesema Serikali imeelekeza kufufua viwanda vyote ambavyo vilibinafsishwa na kutelekezwa na wamiliki wa viwanda hivyo.
“Nichukue nafasi hii kuwaeleza wamiliki wote ambao walibinafsishwa viwanda na kushindwa kuviendeleza sasa ni wakati wa kuviendeleza kabla ya Serikali haijafuatilia,” amesema.
Pia amesema kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia, Wizara ya Viwanda na Biashara imepiga hatua kwa kukuza viwanda vidogo na vikubwa sambamba na kuanzisha uzalishaji wa vifaa vya ujenzi kama vile kiwanda cha nondo,mabati na malumalu.
Amesema katika kukuza na kuboresha viwanda hivyo vimezalisha bidhaa bora, vimeongeza ajira kwa vijana wa kitanzania huku bidhaa hizo zikiuzwa nje ya nchi na Afrika ya kati.
Akielezea mafanikio amesema Serikali imeweza kujenga viwanda vya kutengeneza kioo ambacho kwa sasa kinauzwa ndani na nje ya nchi huku ikiongeza pato la taifa.
Katika hatua nyingine amezungumzia uwepo wa kiwanda cha kutengeneza magari ya kisasa na yenye mwonekano mzuri ambayo yanazalishwa nchini huku akieleza kuwa vipo viwanda ambavyo vinazalisha chuma ambacho kitasaidia kutumika kwenye matengenezo ya magari hayo.
Akizungumzia kiwanda cha General Tyre kilichopo Arusha ambacho  hakifanyi kazi kwa takrikabi miaka 20 sasa amesema Serikali iko kwenye mazungumzo na wawekezaj.
 Uzalishaji wa matairi ulisitishwa mwaka 2007 kutokana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na teknolojia ya zamani, ukosefu wa mtaji, na ushindani kutoka kwa matairi ya bei nafuu yaliyoagizwa kutoka nje ya nchi, hasa kutoka China.

You Might Also Like

UDSM Yamtunuku Rais AfDB Shahada Ya Heshima Ya Sayansi

Madaktari Kutoka Ireland Watoa Matibabu Ya Mifupa Kwa Watoto MOI

Mpango Mkakati wa Takwimu wazinduliwa

Kima Cha Chini Cha Mshahara Chapanda Kwa Asilimia 35.1-Rais Samia

Dkt Biteko Awasili Nchini India Kwa Ziara Ya Kikazi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Baraza La Madiwani Lampongeza Rais Samia Kwa Utekelezaji Wa Ilani
Next Article Serikali Kupeleka Umeme Maeneo Ya Kimkakati
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Dkt. Ikomba wa CWT Aeleza Jinsi Elimu Ilivyobadilisha Taswira ya Tanzania kwa Miaka 64
Habari December 9, 2025
Profesa Ndunguru: Mtafiti Aliyejitoa Kusaidia Dunia Kupata Chakula Cha Baadae
Makala December 9, 2025
Profesa Ndunguru Abainisha Mwelekeo Mpya Wa Mageuzi Ya Kilimo Duniani
Habari December 9, 2025
TPDC na PURA Hakikisheni Watanzania Wananufaika na Rasilimali za Mafuta na Gesi- Salome
Habari December 8, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?