Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 4

China Yafundisha Wanafunzi DIT kuzifikia fursa

 Na Lucy Lyatuu
KAMPUNI ya Ujenzi na Mawasiliano  ya China (CCCC) imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) yenye lengo la kuwajenga ili kuzifikia fursa mbalimbali zilizoko kwenye miradi mikubwa ndani na nje ya nchi.
Wanafunzi waliolengwa ni wa fani ya  uhandisi,sayansi na teknolojia Ili  waweze kujua  yanayohitajika katika kazi watakazozifanya na kuwa na tija zaidi.
Naibu Meneja wa CCCC Tanzania  Liyuliang Lee amesema hayo  Dar es Salaam alipokutana na wanafunzi hao kwa mara ya kwanza katika Taasisi hio Ili kutambulisha Kampuni hiyo ya  kimataifa inayofanya kazi mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Lee amesema Kampuni hio ambayo inamilikiwa na serikali ya China Iko nchini Tanzania tangu 2009 na imekuwa ikijishughulisha na miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo.
Amesema Kampuni imejikita katika shughuli za ujenzi na imekuwa ikiwafikia wahitimu katika vyuo mbalimbali Ili kufundisha fursa mbalimbali zinazopatika  lakini kile kinachotakiwa wanapotafuta ajira.
” Tunawafundisha Ili kuwa na tija na tunaamini kuwa baada ya miaka kadhaa wanaweza kuwa na viwango vikubwa zaidi katika kuchangia uzalishaji wa nchi na kujiongezea thamani,’ amesema Lee.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo Cha Mahusiano Viwandani (DIT) Dk Sosthenes  Karugaba amesema  mafunzo hayo ni kuwaandaa ili kuzifikia fursa mbalimbali katika kampuni za nje.
Amesema  DIT imekuwa ikiwezesha wanafunzi kupata mafunzo viwandani ambayo husaidia walengwa kufanya kazi zao Kwa ufanisi,na kuwa tayari kutumia vifaa vya kisasa.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.