Na Mwandishi Wetu
DODOMA: WATUMISHI wanawake wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Leo Machi saba, 2025 wametembelea Kituo cha Kulea Watoto Miuji Nyumba ya Matumaini Jijini Dodoma kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambayo kilele chake huadhimishwa Machi nane kila mwaka.
Katika ziara hiyo, wametoa msaada wa bidhaa mbalimbali, ikiwemo chakula vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 1.7 kwa ajili ya watoto 65 wanaolelewa kituoni hapo.

Mlezi wa kituo hicho, Sr. Hellen akipokea msaada huo ameishukuru mamlaka hiyo kwa mchango wao.
Akitoa shukrani hizo amesema, kituo hicho hutegemea misaada ya wadau ili kuhudumia watoto wake.
Naye Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa TEA, Alice Lukindo, amesema wanawake wa TEA wameamua kusherehekea siku hiyo kwa kuleta faraja kwa watoto.

“Wanawake tuna wajibu wa kutunza familia na jamii. Leo tumeamua kugusa maisha ya watoto hawa.”
“Kuadhimisha ni kufanya matendo mema,” amesema.