MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Sekta Ya Madini Yapaisha Pato La Taifa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Sekta Ya Madini Yapaisha Pato La Taifa
Habari

Sekta Ya Madini Yapaisha Pato La Taifa

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: TUME ya Madini imeongeza pato la taifa kwa kufikia asilimia tisa  ikilinganisha na asilimia 7.2 kwa mwaka 2021.
Hayo yamesemwa jijini hapa na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Ramadhani Lwamo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na utekelezaji wa tume hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.
Amesema kuwa Tume  ya sekta ya Madini imefanikiwa kuongeza mchango  kwenye Pato la Taifa na kuongezeka  kutoka asilimia 7.2 Mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 9.0 Mwaka 2023.
Lwamo amesema ongezeko hilo limetokana na kuimarika kwa usimamizi wa shughuli mbalimbali za madini.
Vilevile amesema ukuaji wa Sekta ya Madini umeongezeka kutoka asilimia 9.4 Mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 11.3 Mwaka 2023.
“Hii ni Kutokana na kuendelea kuimarika kwa Sekta ya Madini, mwenendo wa Mchango wa Sekta ya Madini na ukuaji wake unatarajiwa kufikia asilimia 10 na zaidi ifikapo Mwaka 2025,”amesema.
Pia amesema kiwango cha  makusanyo ya maduhuli ya Serikali kimepanda kutoka Sh. Bilioni 624.61 zilizokusanywa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia Sh.Bilioni 753.82 mwaka wa fedha 2023/2024
“Kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 mauzo ya madini katika masoko na vituo vya ununuzi wa madini yameendelea kuongezeka kutoka Sh. Bilioni 2.361.80 hadi Shilingi Bilioni 2,597.18 kwa mwaka 2023/2024,”amesema.
Pamoja na hayo amesema Tume ya madini imeendelea kusimamia kikamilifu upatikanaji wa ajira kwa Watanzania kwenye kampuni mbalimbali za uchimbaji wa madini.
Ambapo Ajira 19,874 zimezalishwa na makampuni ya uchimbaji wa madini kati ya hizo, 19,371 ni watanzania.
Ameeleza kuwa Tume imeweka mazingira rafiki kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini kupata leseni za uchimbaji pamoja na kuwaunganisha na taasisi za kifedha ili wapate mikopo kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli za uchimbaji.
“Tume imefanikiwa kutoa jumla ya leseni 41,424 kati ya 37,318 zilizopangwa kutolewa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo ni sawa na asilimia 111. Leseni hizo zilijumuisha leseni za uchimbaji mkubwa, uchimbaji wa kati na uchimbaji mdogo,”amesema

You Might Also Like

COSOTA Yapokea Migogoro 136 Ndani Ya Miaka Minne

Swahili International Tourism Expo Kufanyika Oktoba 11 hadi 13

Tanzania, Uingereza Kushirikiana Kuendeleza madini.

Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija

Wakandarasi Miradi wa  TAZA Watakiwa Kukamilisha Kazi kwa Wakati 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tanzania Yapokea Faru 18 Kutoka Afrika Kusini
Next Article Kassim Majaliwa Mgeni Rasmi Miaka 30 VETA
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
PURA Yajipanga Gesi Asilia Itumike Kwenye Magari
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?