MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania Yapokea Faru 18 Kutoka Afrika Kusini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania Yapokea Faru 18 Kutoka Afrika Kusini
Habari

Tanzania Yapokea Faru 18 Kutoka Afrika Kusini

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mara ya kwanza imepokea Faru weupe 18  kutoka nchini Afrika Kusini kwa lengo la kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii,  Balozi,Dkt.Pindi Chana  ameyasema hayo leo katika hafla ya makabidhiano ya faru hao iliyofanyika katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Mkoani Arusha leo Machi 4,2025.

“Mradi wa kupandikiza faru weupe ndani ya hifadhi ya Eneo la Ngorongoro ni jitihada za kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini na unatekelezwa kwa mara ya kwanza kupitia makubaliano ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kampuni ya AndBeyond” amesema Chana.

Chana amefafanua kuwa katika makubaliano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kampuni ya AndBeyond ilichukua jukumu la kuwezesha upatikanaji na usafirishaji  faru weupe 18 kutoka nchini Afrika Kusini kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili inategemewa kupatikana kwa  faru wengine 18 ili kufikisha jumla ya faru 16 ambapo wengine watawekwa katika maeneo mengine ya uhifadhi nchini.

Chana amemshukuru na kumpongeza  Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jitihda za dhati za kukuza na kuimarisha sekta ya uhifadhi ikiwa ni pamoja na mradi huo wa kupandikiza faru weupe.

Ameweka bayana kuwa Faru weupe ni moja ya wanyamapori ambao wapo hatarini kutoweka na hivyo kuorodheshwa kwenye makundi ya wanyamapori na mimea inayolindwa na Mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyo hatarini kutoweka (CITEs).

Kufuatia hatua hiyo amesema kiu ya Tanzania ni kuunga mkono juhudi za nchi nyingine hususan za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa kuwahifadhi wanyamapori hawa katika mazingira ya asili tofauti na maeneo mengine ambapo hufugwa katika mashamba maalum au bustani.

Amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine Faru weupe watatumika kutoa elimu kwa jamii juu ya usimamizi na uhifadhi wa faru, kuendeleza tafiti zitakazoleta matokeo yatakayoboresha sayansi na uhifadhi wa wanyama hao.

Kwa upande wake Kamishna Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dkt. Elirehema Doriye amesema kuwa kwa kupokea faru hao,Tanzania inathibitisha dhamira yake katika kuilinda spishi ya faru hao walio hatarini kutoweka.

“Faru hawa watachangia juhudi za kimataifa za uhifadhi wa faru, kutoa fursa za tafiti na kitaalamu, kuinua uchumi wa jamii, kukuza utalii na kwamba NCAA imejipanga kuwalinda na kuhakikisha usalama wao” amesema Dkt. Doriye.

Naye, Mwakilishi wa Viongozi wa Kimila kutoka Afrika Kusini, iNkosi Zwelinzima  Gumedeunywano amesema kuwa  lengo la kutoa Faru hao kwa Tanzania ni kuendeleza juhudi za Uhifadhi kwa kuongeza uzalishaji faru katika Afrika Mashariki.

“Tafiti zinaonyesha kwamba faru hawa watakua vizuri na kuzaliana katika eneo la Ngorongoro “amesema Bw. na kusisitiza kuwa wako tayari kutoa ushirikiano kwa Tanzania katika juhudi za uhifadhi.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa Utalii kutoka kampuni ya AndBeyond nchini Afrika Ku

You Might Also Like

Senyamule Ahamasisha Ushiriki Wa Vijana Katika Uchaguzi

Ridhiwani: WCF Umeboresha Mifumo Ya Ushughulikiaji Wa Fidia

Makalla aitaka Halmashauri Longido kutenga fedha, ujenzi wa uzio Samia Girls

VETA Mara Wabuni Mtambo Wa Kuchakata Maji Kwa Samaki Wanaofugwa

TAFIRI Wakabiliana Na Mabadiliko Ya Tabianchi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Makamanda Wa Polisi Msiende Nyumbani na Vyeo Vya Ukamanda
Next Article Sekta Ya Madini Yapaisha Pato La Taifa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?