MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kasi Ya Kusambaza Umeme Kwenye Vitongoji Yaanza-Kapinga
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kasi Ya Kusambaza Umeme Kwenye Vitongoji Yaanza-Kapinga
Habari

Kasi Ya Kusambaza Umeme Kwenye Vitongoji Yaanza-Kapinga

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
NAIBU  Waziri wa Nishati,  Judith Kapinga amesema  hadi kufikia Januari, 2025, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imekamilisha upelekaji wa umeme kwenye vijiji vyote 12,318 nchini na kwamba kazi inayofanyika sasa ni kuendelea kusambaza umeme vitongojini.
 Kapinga ameyasema hayo leo Februari 4, 2025 bungeni jijini Dodoma  wakati akijibu swali  la Mbunge wa Viti Maalumu  Jacquelune Andrew aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itamaliza  kusambaza umeme kwenye Vitongoji nchini.
“Serikali imepeleka umeme kwenye vitongoji 33,657 kati ya vitongoji 64,359 sawa na asilimia 52.3”, Amesema  Kapinga
Ameongeza kuwa, Vitongoji 30,702 vilivyobaki vitapata umeme kupitia mpango wa miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji ambapo tayari Serikali imeshaandaa Mpango wa kupeleka umeme katika vitongoji 20,000 kwa kipindi cha kati ya miaka mitano  hadi 10 kuanzia Mwaka wa Fedha 2023/24.
Kapinga ameongeza kuwa,  vitongoji 4,020 tayari vipo katika Mpango wa utekelezaji kupitia miradi mbalimbali.
Akijibu swali la Mbunge wa Kilindi,  Omar Kigua aliyeuliza ni upi mpango wa Serikali kufikisha umeme kwenye maeneo yote ya uchimbaji wa madini Kilindi,  Kapinga  amesema Wilaya ya Kilindi ina maeneo yapatayo 12 ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ambapo kati ya hayo, maeneo 4 tayari yameshapatiwa huduma ya umeme.
Ameyataja maeneo yenye umeme kuwa  ni Mafulila, Mfyalime/Najim,  Masagulu Muheza na Chanungu.
Aidha, eneo la Matanda, mkandarasi aitwae DIEYNEM Co. Ltd anaendelea na kazi ya kuweka miundombinu ya umeme na anatarajia kukamilisha kazi hiyo hivi karibuni.
Kapinga amesisitiza kuwa maeneo mengine ya migodi yaliyosalia yatapata umeme kupitia miradi mbalimbali itakayofuata.
Kuhusu utekelezaji wa mradi wa gridi imara katika maeneo ya Mkata na Kilindi  Kapinga amesema  wanaendelea na mazungumzo na Wizara ya Fedha kwa ajili ya kupeleka fedha za kutekeleza mradi huo.
Akijibu swali Mbunge wa Kiteto,  Edward Olelekaita aliyetaka kufahamu kauli ya Serikali kutokana na  wananchi kuunguza vifaa kwa sababu ya kukatika kwa umeme,  Kapinga amesema Serikali inao utaratibu wa kuwalinda watumiaji wa umeme kupitia EWURA na kutoa rai kwa mwananchi ambaye amepata athari kushughulikia malalamiko kupitia EWURA.
Akijibu swali la Mbunge wa Iringa, Jesca Msambatavangu aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanza  kusambaza umeme kwenye mitaa 15 ya kila majimbo ikiwemo Iringa Mjini mtaa wa Mtalagala na Msisima,  Kapinga amesema tayari Mkandarasi yupo eneo la kazi na ameshamaliza uhakiki.
Aidha, kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amelielekeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuja na mkakati wa kuwa na nguzo za chuma ili zikae maeneo ya milimani.

You Might Also Like

Kamati Ya Bunge Yapongeza Usimikaji Mfumo Wa Kidijitali CMA

UDSM Imekuja Na App Inayounganisha Wakulima na Watoa Huduma za Kilimo kwa Haraka

Zimbabwe Yakabidhi Uenyekiti Kwa Madagascar

TRAWU Kupambania Mkataba Wa Hali Bora Kwa Wafanyakazi

Sera mpya ya viwanda kuzinduliwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Chanzo Cha Bunge Kuridhia Hoja Ya Wanaojifungua Njiti, Kilianzia Hapa
Next Article Wanafunzi Wawili Wajiteka Ili Wapate Pesa Toka Kwa Wazazi wao
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?