MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wapongeza Nyongeza Ya Likizo Kwa Aliyejifungua Mtoto Njiti
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wapongeza Nyongeza Ya Likizo Kwa Aliyejifungua Mtoto Njiti
Habari

Wapongeza Nyongeza Ya Likizo Kwa Aliyejifungua Mtoto Njiti

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu
CHAMA cha  Wafanyakazi Wa Serikali Na Afya Tanzania (TUGHE) kwa kushirikiana na  wadau mbalimbali wamepongeza hatua ya serikali  kupitisha  sheria kuwa  likizo ya uzazi kwa mwajiriwa aliyejifungua mtoto njiti kujumuishwa  kuwa wiki 40 za ujauzito.
Aidha sheria hiyo imepitisha baba kupewa nyongeza ya likizo ya uzazi kutoka siku tatu na kuwa siku saba kwa wafanyakazi waliojifungua mtoto njiti.
Pongezi hizo zimetolewa Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Tughe , Dk Jane Madete kwa kushirikiana na mtandao wa haki ya afya ya uzazi na taasisi ya Doris Mollel Foundation.
Akizungumza Madete amesema suala la nyongeza ya uzazi kwa wafanyakazi waliojifungua mtoto njiti lilikuwa ni maombi ya muda mrefu yaliyoasisiwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation tangu mwaka 2017 na baadae mwaka 2023 kuungana na mtandao wa haki ya afya   pamoja na Tughe ili kuhakikisha suala hilo libakubalika.
Aidha amesema Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi  Tanzania (TUCTA ) lilibeba suala hilo na mwaka jana 2024  liliwakilishwa kwenye siku ya Wafanyakazi  ambapo Januari 31,2025 serikali ilipitisha rasmi  kuwa sheria.
“Kwa pamoja tumekuja kutoa pongezi  za shukrani  pamoja na Bunge la Jamhuri ya Tanzania  kupitisha maombi hayo kuwa sheria kuanzia sasa, ” amesema.
Amesema akiwasilisha Bungeni  maelezo ya Mswaada wa marekebisho ya sheria za kazi namba 13 wa mwaka 2024,Waziri wa Madini  Anthony Mavunde kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira Na Wenye Ulemavu, Ridhiwan Kikwete  alieleza kuwa kuanzia sasa mfanyakazi atakayejifungua mtoto njiti likizo yake itaisha  baada ya kufikisha wiki 40 ya ujauzito  na baba kupewa siku saba za mapumziko.
Madete amesema kwa pamoja TUCTA, TUGHE na Taasisi ya Doris Mollel na Mtandao wa HakibYa Afya Ya Uzazi tunapongeza hatua hiyo kwani itasaidia  kuimarisha ustawi wa mfanyakazi.
Amesema kabla ya sheria hiyo ilikuwa ni changamoto kwa mfanyakazi ikiwemo ya afya kwani wanahitaji muda mwingi wa kupumzika pia kuhudumia mtoto tangu kipindi cha uangalizi anaporuhusiwa kutoka hospitali.
“Mbali na changamoto hiyo ya kiafya pia wamekuwa wakipoteza ajira zao jambo linalosababisha kupata msongo wa mawazo hata kuathiri malezi ya mtoto aliyezaliwa, ‘ amesema.
Amesema kufuatia nyongeza hiyo ya likizo itasaidia wanawake hao kupata muda wa kutosha kuhudumia mtoto kwa kipindi chote bila kuwa na wasiwasi na kupoteza ajira.
Amesema na akiwa kazini afya itakuwa imara na kufanya kazi kwa tija hivyo wanaipongeza serikali kwa hatua hiyo.

You Might Also Like

Wanafunzi Msingi Wajitosa Kujifunza Kichina

Wenye Ulemavu Wa Ngozi Wakumbukwa Kupitia FDH, Wapewa Msaada Wa Milioni 20

Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Wanaotumika Vibaya Waonywe

Kampeni ya Mama Samia imewafikia zaidi ya watu 4000 mikoa saba

Rais Mwinyi adhamiria kusimamia ubora wa bidhaa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Usajili Kwa Njia Ya Mtandao, Umeharakisha Ufunguaji Mashauri
Next Article Chanzo Cha Bunge Kuridhia Hoja Ya Wanaojifungua Njiti, Kilianzia Hapa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?