Na Lucy Lyatuu
UBALOZI wa Italia Tanzania pamoja na Wakala wa Biashara wa Italia (ICE) kwa kushirikiana na Wizara Ya Mambo Ya Nje na Ushirikiano Wa Afrika Mashariki kupitia Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wameandaa kongamano la kibiashara litakaloangazia fursa za uwekezaji ambazo hazijatambuliwa na kutumika kikamilifu nchini Tanzania.
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika nchini kwa siku mbili kuanzia Februari 11 =12 likiwa na wawekezaji zaidi ya 40 kutoka nchini Italia,tukio ambalo litawezesha kukuza kukuza biashara na uwekezaji,
Akizungumza leo Dar es Saalam, Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji Kimataifa kutoka TIC, John Mmali amesema kongamano hilo linatarajiwa kuvutia ushiriki wa mamlaka kutoka Tanzania na Italia,mashirika ya sekta binafsi, mitandao ya biashara ya kikanda na vyama vya ushirika.
Amesema madhumuni ya kongamano ni kukuza biashara baina ya pande mbili,kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji na kujenga mitandao ya kibiashara kupitia mijadala ya wazi,warsha za kitaalam na ziara kibiashara zenye dhumuni la kutoa mafunzo na kushirikisha ujuzi ujuzi na maarifa jambo litakalosaidia wadau kuelewa hali yamuchumi,mitazamo ya kibiashara na kuimarisha mahusiano thabiti na wadau huku wakitafuta fursa za uwekezaji katika sekta tofauti.
Kwa upande wake Balozi wa Italia nchini, Giuseppe Coppola amesema kongamano litaangazia fursa za uwekezaji ikiwemo teknolojia za kilimo na uchumi wa buluu ikihusisha utaalamu kwenye masuala ya mbolea mifumo ya umwagiliaji , ufugaji, matumizi ya ngozi, ufugaji wa samaki na usambazaji.
KadhaIka amesema eneo lingine litakaloangaziwa ni uchumi wa kijani na miundombinu endelevu, uzalishaji wa nishti safi kutokana na ta, nishati mbadala,kemikali za kusafishia maji,usafirishaji,miundombinu endelevu,maendeleoo ya kidigitali na madini.
Balozi amesema eneo lingine ni sekta ya afya na dawa,teknolojia za afya, mashine, huduma za kiafya,vifaa vya meno ,vifaa vya michezo na huduma nyinginezo.
Amesema Tanzania inasafirisha bidhaa za kilimo.madini na maliasili kama vile kahawa, chai, Pamba,samaki,madini na Vito vya thamani kwenda Italia huku nchi hiyo ikionesha nia ya dhati ya kuwekeza Tanzania katika sekta ya utalii na kilimo.
Kamishna wa Biashara ICE,Claudia Pasqualucci amesema mahusiano ya Tanzania na Italia yameendelea kukua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni,biashara baina ya nchi hizo zimeimarika kwa kiasi kikubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda,ki.imo,utalii,ushirikiano wz kiufundi,mashi e,kemikali,vifaa vya umeme,dawa na bidhaa za chakula.