Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 4

Serikali Kuboresha , Kuweka Mazingira Wezeshi Kwa Vijana

Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Ridhiwani Kikwete amesema Serikali imejidhatiti kuweka mazingira yanayowezesha vijana kutoka kwenye uchumi usio rasmi kuelekea uchumi ulio rasmi.
Ridhiwani amesema hayo wakati wa uzinduzi wa uchambuzi wa kina wa sekta isiyo rasmi katika biashara zinazoongozwa na Vijana jijini Dar es Salaam.
Amesema serikali inaendelea kuimarisha sera zinazowezesha nguvu kazi ya taifa, kuondoa vikwazo, kutoa msaada wa kiufundi  na kifedha kwa Vijana.
Kwa maelezo ya Ridhiwani tafiti zilizofanywa sekta zisizo rasmi zitasaidia kupata majawabu ya matatizo ya Vijana katika kukabiliana na changamoto isiyo rasmi.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkurugenzi  wa Shirikia la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki, Caroline Mugalla, pamoja na watendaji wengine.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.