Na Mwandishi Wetu
SERIKALI inatarajia kuzindua Mpango Kazi wa Kupambania Haki za Wenye Ulemavu siku za karibuni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amesema hayo katika matembezi yanayojulikana kama Sunset Walk aliyoshiriki.

Matembezi hayo yanaunga mkono taasisi inayosimamia haki za wenye Ualbino (TAS) na Lions Club kwa ajili ya kuchangia fedha zitakazosaidia kupatikana kwa mahitaji muhimu yakiwemo mafuta ya ngozi, kofia kinga na mengineyo.
Ridhiwani amesema uzinduzi wa mpango kazi huo ni moja ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali.


