DAR ES SALAAM: .HAKUNA chama kingine cha siasa zaidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilichosimamisha nchi katika mchakato wa kura za maoni wa kuwania nafasi katika chama hicho, katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema hayo leo Mkoani Dar es Salaam.
Amesema ni wazi kura za maoni ndani ya chama hicho zilisimamisha nchi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, hivyo walichukulia changamoto zilizojitokeza kuwa ni changa kwenye chama kikubwa kama CCM.
“Na yale ambayo yako ndani ya uwezo wetu tuliendelea kuyatatua. Tunawaahidi watanzania wote kuwa na wana CCM kura za maoni zimeisha tunakwenda kwenye uteuzi wa wagombea na wote tuwaombe twendeni tuwe kitu kimoja,” amesema.