Na Lucy Lyatuu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu) , Ridhiwan Kikwete amesema kanuni kwa ajili ya program ya marekebisho kwa Sheria ya fidia kwa wafanyakazi wanapopatwa na majanga sehemu za kazi zimekamilika zenye kuboresha mazingira kwa Mfanyakazi.
Program hizo ni zile zenye kuhudumia wafanyakazi wanapopata na tatizo wakiwa kazini ili waweze kuandaliwa au kujiandaa vizuri nje au ndani ya maisha ya kazi.
Ridhiwan amesema hayo jijini Dodoma mbele ya Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA),Tumaini Nyamhokya alipofanya ziara rasmi ya kutambulisha gazeti la MFANYAKAZI akiongozana na Mhariri Mkuu Shani Kibwasali .

Kuhusu kanuni hizo Ridhiwan amesema Serikali inafanya juhudi kubwa kutekeleza matakwa ya wafanyakazi hivyo amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF ), Dkt. John Mduma ili kuzungumzia sheria zilizopitishwa Bungeni hivi karibuni.
“Nilitoa agizo kwa taasisi zote zilizo chini ya Wizara kuwa kila Taasisi itengeneze program kwa ajili ya kutekeleza sheria moja baada ya nyingine” amesema na kuongeza,
“Hivyo nimemuita Mkurugenzi wa WCF na kujadili kuwa kwenye mabadiliko ya Sheria Wafanyakazi wanaopata majanga kazini kama kuvunjika miguu na kutumia viungo bandia wawe wafanyakazi wenye mustakabali wa mwingine kwa kuboreshewa zaidi mazingira “, amesema.
Amesema chini ya program hiyo ni kuandaa kwa upya kwamba iwapo dereva aliyepata ajali,sheria zilizopo zinaweza kumnufaisha na kwamba fidia na maisha yake baada ya majanga yakoje ama ndio anaweza kubadilika kabisa.
“Chini ya program ya kanuni mpya mfanyakazi atazingazitiwa ni Kwa namna gani analindwa na fidia na kwamba maisha yake yanaweza kubadilika,” amesema Ridhiwani na kuongeza kuwa WCF awali walikuwa na program moja pekee ikiwemo ya kumuangalia mfanyakazi kiafya .

Amesema kwenye hio program Mfanyakazi akipata shida ya miguu anavalishwa ya miguu ya bandia ama jicho la bandia,lakini kwenye maeneo ya saikolojia unakuta Hilo jambo halipo pia kwenye suala la afya ya akili, ambapo hizo program zinakwenda kubadilika chini ya kanuni hiyo.
Ridhiwan amesema amemuagiza Mkurugenzi wa WCF kuandaa timu ya Wanasheria Ili kupitia pamoja na Katibu Mkuu Ili Sheria hiyo ipitishwe.
‘ Huu ni ushindi mkubwa Kwa wafanyakazi na zitakaposainiwa Mfanyakazi popote alipi atambue nna serikali inatwkelwza matakwa yao.