MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: CMA yawataka wafanyakazi walioachishwa kazi kuwasilisha mgogoro ndani ya muda
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > CMA yawataka wafanyakazi walioachishwa kazi kuwasilisha mgogoro ndani ya muda
Habari

CMA yawataka wafanyakazi walioachishwa kazi kuwasilisha mgogoro ndani ya muda

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
WAFANYAKAZI wametakiwa kuwasilisha migogoro ya kikazi ndani ya siku 30 katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), tokea walipoachishwa kazi.
Ofisa Mfawidhi CMA, Yohana Massawe amesema hayo alipozungumza na Mfanyakazi.
Massawe amesema, “Migogoro yote inayowasilishwa mbele ya tume hiyo, inapaswa kuwasilishwa ndani ya wakati, migogoro inayohusu uachishwaji wa kazi inapaswa kuwasilishwa ndani ya siku 30 tangu mfanyakazi husika alipoachishwa kazi.

“Mfanyakazi atakapochelewa kuwasilisha huo mgogoro ndani ya siku 30 anatakiwa kuomba au kuwasilisha maombi ya kusikilizwa nje ya muda,” amesema.

Amesema kwenye maombi hayo mhusika atatakiwa kuweka taarifa ya maombi itakayoambatana na kiapo, pia kama kuna viambatanisho vingine ikiwa vinaisaidia fomu namba mbili ya kusikilizwa nje ya muda navyo vinawasilishwa.

Pia amesema migogoro mingine yote nje ya uachishwaji wa kazi inapaswa kuwasilishwa ndani ya siku 60 ikiwa ni pamoja na madai ya mishahara na migogoro mingine yoyote ambayo mfanyakazi anaona inahitaji utatuzi wa tume hiyo.

Amesisitiza kuwa, ni muhimu kwa wafanyakazi kuzingatia suala hilo la muda, kwa sababu pamoja na kwamba kuna huo mlango wa kupeleka maombi nje ya muda lakini bado mhusika ana wajibu wa kueleza sababu za msingi kwa nini alichelewa kufungua mgogoro.

“Kuchelewa haijalishi ni muda gani hata kama ni siku moja unatakiwa uielezee ile siku moja umechelewa kwa sababu gani na usipoweza kutoa sababu za msingi pia maombi hayo hayataweza kupokelewa na hivyo mfanyakazi unajikuta unakosa haki zako za msingi haki ambazo ungeweza kuzipata kwa kuwasilisha mgogoro ndani ya wakati.

“Lakini katika kuwasilisha maombi kuna vitu vya kuzingatia pamoja na taarifa ya maombi na hati ya kiapo lakini katika hiyo hati ya kiapo lazima ueleze ulichelewa kwa muda gani kwa maana idadi ya siku lazima uzitaje lakini katika hizo siku ulizozitaja umechelewa kwa sababu gani,” amesema.

Amesema sababu zitakazotolewa lazima zithibitishe kweli kila siku iliyozungumziwa ina sababu ya msingi ambayo itasikilizwa na tume.

“Kwa hiyo msisitizo ni kwamba wafanyakazi wanapaswa kuelewa msingi wa sheria, na sheria haina huruma ni msumeno lazima uizingatie,

“Lazima uitekeleze inavyokutaka ufanye kwa yeyote mwenye kudai haki yake anapaswa kuitafuta kwa wakati , usipoitafuta hakuna atakayekuletea haki yako nyumbani,”amesema.

 

 

 

You Might Also Like

Dkt Biteko Awasili Nchini India Kwa Ziara Ya Kikazi

Trilioni 1.3  Zatumika Kuboresha Afya Ya Msingi Nchini

Watahiniwa 72 wa kidato cha nne wafutiwa mtihani kwa udanganyifu, kuandika lugha za matusi

TARI Yaja Na Jawabu 88 Juu Ya Tindikali, Chumvi Kwenye Udongo

Ridhiwan Kikwete awaagiza maofisa kazi kushirikiana na WCF

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Thamani ya Fedha Ionekane Kwenye Utekelezaji wa Miradi-Nyamoga
Next Article Wasilisheni Migogoro Yenu Tume ya Usuluhishi na Uamuzi – Massawe
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Nishati Safi Kwa Kila Mtanzania Inawezekana – Saidy
Habari August 7, 2025
Bodi ya Maziwa Yatoa Mafunzo ya Ubora, Usalama wa Maziwa Katika Maonyesho ya Nane Nane
Habari August 7, 2025
Balozi wa Tanzania Nchini Italy Afurahishwa  Ubunifu wa TPHPA Maonesho ya Nanenane
Habari August 7, 2025
Wadau Wakaribishwa Kuwekeza Katika Uchakataji, Biashara ya Mkonge Nchini
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?