Na Lucy Lyatuu
KAMATI ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imelielekeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kutatua changamoto zinazowakumba ikiwemo suala zima la deni.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwanaisha Khamisi Juma amesema leo Dar es Salaam wakati Kamati hiyo ilipotembeleà Shirika Hilo kuona wanavyofanya kazi kama sehemu ya taasisi za Muungano.
Amesema Pamoja na mambo mengine waliyojadiliana wamewashauri kukaa pamoja Ili kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikumba Shirika Hilo kwani ni mambo ya kimuungano.
” Pamoja na mengi mazuri yaliyofanywa na Shirika hili lakini kwenye mafanikio hakukosi changamoto hivyo wakae pamoja ili kuzitafutia Suluhu,”amesema Mwenyekiti Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo bila kufafanua zaidi kuhusu deni.
Hata hivyo amesema Kamati hiyo imeridhika na kinachofanywa na Shirika Hilo pamoja na jitihada zinzofanywa na Marais wote Kwa kuhakikisha wanaweza miundombinu imara.
Kadhalika amelitaka Shirika Hilo kuhakikisha wanatoa gawio Kwa serikali pindi muda wa kufanya hivyo utakapofikiwa kwani ni eneo linalorudisha tija kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TTCL, Moremi Marwa amesema wamepata maelekezo na watayafanyia kazi kama inavyostahili.
Mbali ya majadiliano hayo,Kamati hiyo imetembelea kituo Cha uangalizi na uendeshaji wa mtandao na miundombinu ya mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.