MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania Ipo Tayari Soko la Pamoja kuuziana Umeme – Biteko
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania Ipo Tayari Soko la Pamoja kuuziana Umeme – Biteko
Habari

Tanzania Ipo Tayari Soko la Pamoja kuuziana Umeme – Biteko

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na Mwandishi Wetu, Kampala, Uganda
TANZANIA  imejipanga vema kuhakikisha inatumia fursa ya uwepo wa soko la pamoja la mauziano ya umeme kwa nchi wanachama wa soko la pamoja la nchi za Mashariki mwa Afrika ( EAPP ) .
Fursa hiyo ni pamoja na  kuhakikisha inaunganisha miundombinu yake ya kusafirisha umeme na nchi wanachama wa EAPP.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati wa mkutano wa 19 wa nchi wanachama wa umoja wa mauziano ya umeme EAPP uliowakutanisha Mawaziri wa Nishati na Makatibu Wakuu nchini Uganda.
Mkutano huo  umezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kupitisha mabadiliko ya muundo wa kiuongozi wa EAPP, kuridhia kanuni na taratibu za kiuendeshaji za EAPP .
Kadhalika umeridhia   uwepo wa kitengo huru cha masoko kinachojitegemea kusimamia soko la pamoja la mauziano ya Umeme kwa nchi wanachama.
‘”Nafurahi kuona kuwa tumefikia muafaka kwenye masuala ya msingi kwenye kikao cha Mawaziri wa Nishati  hususani uwepo wa kitengo huru cha Masoko kinachojitegemea  kwa ajili ya kusimamia mauziano ya umeme.
Na kwakuwa Tanzania tutakuwa na umeme kutoka mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere  tutatumia vema fursa hiyo kuwauzia umeme nchi wanachama pale tutakapokuwa na ziada na sisi kununua tutakapokuwa na upungufu’’ amesema Dkt. Biteko.
Katika kufanikisha hilo Dkt. Biteko amesema tayari miundombinu wezeshi inaendelea kuwekwa kupitia Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ili kujiandaa kuingia kwenye soko la pamoja ambapo laini kubwa ya kuunganisha Tanzania na Kenya kupitia Namanga imeshajengwa na imekamilika.
Amesema laini  ya kuunganisha Tanzania na Zambia- TAZA imeshaanza kujengwa na itakamilika ifikapo 2026.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa sasa wa soko la pamoja la kuuziana umeme la nchi za kaskazini Mashariki EAPP na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini nchini Uganda . Dkt. Ruth Ssentamu amesema EAPP imeridhia ushiriki wa Makatibu Wakuu wa Nishati kutoka nchi wanachama kushirikishwa katika muundo wa kiutawala wa EAPP.
Amesema kuundo huo ni  kwa ajili ya kusaidia kuchakata na kupitia taarifa kutoka kwa watendaji wa kisekta kabla ya kupelekwa katika kikao cha baraza la Mawaziri la nchi wanachama ili kutolewa maamuzi.
Aidha, Mhe Ssentamu amesema maadhimio hayo yamefikiwa kufuatia makubaliano ya mkutano wa 18 wa baraza la mawaziri ulioanyika nchini Kenya kuhusu umuhimu wa kupitia mapendekezo ya uendeshaji wa shughuli za EAPP.
Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Felchesmi Mramba amesema pindi uuzaji wa umeme kwenye soko la pamoja utakapoanza utatoa nafasi za ajira kwa nchi wanachama wa EAPP pamoja na kubadilishana wataalamu hususan kwenye miradi ya kusafirisha umeme na  kuiongezea TANESCO mapato.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo wa Baraza la Mawaziri wa Nishati uliongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati  Dkt. Doto Biteko, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki,   Dennis Londo, Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati  Felchesmi Mramba.
Wengine ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mha. Gissima Nyamo-Hanga, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mipango, Utafiti na Uwekezaji TANESCO CPA Renata Ndege, viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

You Might Also Like

Wafanyakazi Wakumbushwa Kujitokeza. Kwa Wingi Kupiga Kura

Mpogolo Aipongeza Halmashauri Maandalizi Mikopo Asilimia 10

Maabara Za Sayansi Zachochea Hamasa Kitaaluma

Bajeti ya TUGHE 2025 Yaidhinishwa

Dhibitini Magonjwa ya Mlipuko-Mchengerwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Magonjwa ya misuli yaongezeka mahala pa kazi-OSHA
Next Article Ridhiwani akutana na Mtendaji Mkuu ATE
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

UDSM Yatafiti Ndege Nyuki ‘Drone’ Inayopunguza Uchafuzi Wa Hewa Ukaa
Habari May 29, 2025
Mtafiti UDSM Atafiti Mimea Ya Asili Kudhiti Fangasi Kwenye Mimea
Habari May 29, 2025
Ridhiwani Afanya Mazungumzo Na Balozi Wa China Nchini, Mingjian
Habari May 29, 2025
Kafulila: Deni La Taifa Ni Himilivu
Habari May 29, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?