MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali kushirikiana na Wadau usimamizi Taka za Plastiki
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali kushirikiana na Wadau usimamizi Taka za Plastiki
Habari

Serikali kushirikiana na Wadau usimamizi Taka za Plastiki

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU  wa Rais  Dkt. Philip Mpango leo Agosti 15 ,2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Sekretariet ya Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano katika Usimamizi na Menejimenti ya Taka za Plastiki  Clemence Schmid, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesema serikali imedhamiria kushirikiana na wadau, sekta binafsi pamoja na jumuiya ya kimataifa katika kupambana na tatizo la taka za plastiki nchini.
Amesema uzoefu unaonesha kwamba ushirikiano ni njia bora zaidi itakayowezesha kukabiliana na tatizo hilo kwani yapo maeneo ambayo taka za plastiki hutupwa na kufika katika mataifa mengine hususani kwa njia ya bahari.
Amewakaribisha Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) kupitia Ushirikiano wa Kimataifa katika Usimamizi na Menejimenti ya Taka za Plastiki kushirikiana na Tanzania katika mbinu mbalimbali za kukabiliana na uchafuzi wa taka za palstiki kama vile kuwajengea uwezo wataalamu,
Pia kuwezesha teknolojia na vifaa vya kisasa vya urejerezaji wa taka za plastiki pamoja na ufadhili wa kifedha katika miradi ya kukabiliana na uchafuzi wa taka za plastiki.
Makamu wa Rais amesema Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na taka za plastiki kama vile kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki pamoja na utoaji elimu ya kuhamasisha wananchi kubadili tabia ya utupaji taka za plastiki ovyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano katika Usimamizi na Menejimenti ya Taka za Plastiki wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF)  Clemence Schmid ameipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada na nia ya dhati ya kupambana na taka za plastiki.
Amesema ujumbe wa Sekretarieti ya Jukwaa la Uchumi Duniani umejionea dhamira ya dhati ya Tanzania katika kutoa kipaumbele cha juu kuzuia uchafuzi wa mazingira husasani wa taka za plastiki.
Ametaja vipaumbele katika ushirikiano huo ni pamoja na kutambua changamoto zilizopo, kuwaunganisha wadau pamoja na kutambua namna ya kutumia rasilimali fedha na uwekezaji katika kuandaa miundombinu rafiki ya kutumia vema taka za plastiki kiuchumi.

You Might Also Like

Dkt. Bwana: Tunafanya utafiti wa mbegu kutatua changamoto za wakulima

Ridhiwani Ashiriki Kikao Cha Kazi Na Ajira Saudi Arabia

Dkt Yonaz Awaasa Watumishi Ofisi Ya Waziri Mkuu  Kuongeza Bidii Katika Kutekeleza Majukumu Yao

Kamati Ya Bunge  Yaridhishwa Na Ujenzi Wa Jengo La Kituo Cha Zimamoto, Mtumba

VETA Kihonda Waja Na Mashine Ya Kusaga Chumvi Sabasaba

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Chalamila afanya ukaguzi mwenendo wa utoaji huduma Kivuko cha Feri
Next Article Asali inayozalishwa nchini kukidhi ubora wa kimataifa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tulia Atoa Taarifa Kifo Cha Ndugai
Habari August 6, 2025
Tume ya Kurekebisha Sheria Yaelimisha Umma Kuhusu Haki za Wanyama
Habari August 6, 2025
Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima
Habari August 6, 2025
Ofisa wa TARI Kuwapo Kila Kituo cha Umwagiliaji – Naibu Katibu Mkuu
Habari August 6, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?