Na Lucy Ngowi
DODOMA:MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imeweka vituo vya hali ya hewa kwenye Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (REA).
Meneja Huduma za Hali ya Hewa Kilimo TMA, Isack Yonah amesema hayo wakati wa maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayofikia kilele leo jijini Dodoma.
Amesema kazi ya vituo hivyo ni kutoa taarifa za hali ya hewa kwa ajili ya utafiti wa mazao yanayoweza kuendana na kilimo cha sasa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Amesema katika kuboresha huduma zao wameweka vituo vinavyojiendesha vyenyewe na kuachana na teknolojia ile ya zamani ambayo mtu anakwenda anaangalia na kutoa utafiti ambao pengine anaweza kukosea kusoma, au wakapita wanyama wakaharibu.
Amesema vituo hivyo walivyoweka vinajiendesha vyenyewe, inachukua takwimu na kuziongoza kwenye mifumo ya utabiri na kupata utabiri ambao ni bora zaidi, hivyo kusaidia kilimo na wakulima kwa ujumla.
“Kwa hiyo Mamlaka na Serikali kwa ujumla inawekeza sana kwa vifaa na mitambo ili kuhakikisha kwamba utabiri unatolewa ni wa uhakika .”amesema.
Amesema katika maonesho hayo wanaelimisha wananchi kwa huduma wanazozitoa kwa sekta ya Kilimo na sehemu nyingine za uchumi.
“Kwa hiyo tumekuja hapa ili kujibu baadhi ya maswali yanayoulizwa na wananchi lakini pia watupe mahitaji yao ili kilimo chao kiweze kuwa bora kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo huathiri mazao ya wakulima,