MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Silinde: Serikali bega kwa bega na wadau wa kilimo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Silinde: Serikali bega kwa bega na wadau wa kilimo
Habari

Silinde: Serikali bega kwa bega na wadau wa kilimo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: NAIBU Waziri wa Kilimo David Silinde amewataka wadau wa kilimo kushirikiana na serikali katika kuwarahisishia wakulima kufanya shughuli zao kisasa.
Silinde amesema hayo baada ya kugawa matrekta tisa kwa wakulima waliopatiwa mkopo wa vitendea kazi hivyo, alipotembelea banda la Agricom katika maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea Jijini Dodoma.
Pia amewataka wadau mbalimbali kuiga mfano wa taasisi ya  Pass Leasing ambayo imetoa matrekta  kwa wananchi tisa yatakayowarahisishia kilimo.
 Katika banda hilo la Agricom ambapo wanufaika wa matrekta hayo walikuwa ni wanawake na vijana,  Silinde amesema serikali itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau hao wa kilimo kwa kuwa haiwezi kufanya kila kitu pasipo ushirikiano kama huo.
“Pass Leasing  tunawashukuru kwa kazi mnayofainya ya kuwawezesha wananchi zana hizi za  kilimo ,na  hili ni jambo ambalo sisi kama serikali tutaendelea kuwaunga mkono. Tunahitaji wadau kama ninyi kuhakikisha hii sekta ya kilimo tunaisogeza pamoja.
“Na siku zote tumekuwa tukizungumza kwamba Sisi kama Wizara hatulimi,wanaolima ni wananchi na kilimo ni sayansi ambayo inahitaji ushirikiano wa pamoja ili kwenda mbele,kwa hiyo kwa kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ana dhamira ya dhati kuhakikisha kwamba kilimo tunakibadilisha kwenye viwango vingine,” amesema.
Amesema wizara hiyo imekusudia kutumia teknolojua za kisasa zitakazowarahisishia wakulima, kuachana na ulimaji wa jembe la mkono, lakini kufanya kilimo cha umwagiliaji pasipo kutegemea mvua kwa kujenga mabwawa ya umwagiliaji ili wananchi walime kwa tija.
Kwa upande wake Mkurugenzi Bodi ya Pass Leasing Rosebad Kurwijila amesema taasisi hiyo itawawezesha wakulima kupata zana za kilimo ili waweze kuzalisha kwa tija.
“Na tunapotoa vifaa hivi tunazingatia mnyororo wa thamani tangu kulima mpaka kuyaandaa mazao ,na mpaka sasa tumeshawawezesha wakulima 1,000.”amesema.
Baadhi ya wakulima waliokabidhiwa matrekta hayo  wameishukuru PASS Leasing kwa kuwapatia mkopo huo ambao utawasaidia kuongeza tija kwa kulima kisasa na kuachana na jembe la mkono.

You Might Also Like

Rafiki Planter’Teknolojia Rahisi, Tija Kubwa”

Serikali Yaimarisha Mafunzo Ya Vitendo Kupitia Ushirikiano, Viwanda

TOSCI: Mbegu Bora Ni Ajira, Biashara

TFS Yashiriki Maonesho ya Nane ya Madini Geita

DC Atoa Wito kwa Tume ya Kurekebisha Sheria Kuzingatia Sheria Ndogondogo za Halmashauri

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mwenda: Tupo kwa ajili ya kuzitatua changamoto za wananchi
Next Article Wazazi washauriwa kusomesha watoto useremala
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Yatoa Mwelekeo Maandalizi AFCON 2027, Yaimarisha Miundombinu Nchini
Habari April 17, 2026
Makampuni 100 kushiriki maonesho ya OSHA Njombe
Habari April 17, 2026
Ufaulu  Wa   Somo La Hisabati  Shida Ya Taifa- Wanu
Habari April 16, 2026
Ofisi ya Rais Mipango Yaomba Bilioni 144.85 kwa Bajeti 2026/27
Habari April 16, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?