Na Lucy Lyatuu
SHIRIKA la Maendeleo la Taifa (NDC) limesema mradi wa kwanza wa kuzalisha chuma nchini na Afrika Mashariki wa Maganga Matitu unatarajiwa kuanza utekelezaji Januri 2025, tayari mwekezaji amepatikana huku uwekezaji wake ukifikia dola milioni 77.4.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Nicolaus Shombe amesema hayo leo Dar es Salaam mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara alipotembelea shirika hilo kuzungumza na wafanyakazi.
Amesema mkataba kwa ajili ya kuanza kwa mradi huo utasainiwa ijumaa wiki hii(Agosti 2,2024) na wanatarajia kuanza kuchimba kiasi cha tani milioni moja kwa mwaka lakini kadri uwekezaji unavyoendelea wanaweza kuongeza pia.
Amesema mwekezaji anaaza kulipa fidia watu waondoke na kuweka mashimo Kwa ajili ya kuanza.
” Mkataba wa mradi huu una mpango wa utekelezaji kwamba mwekezaji asipotekeleza mkataba unaweza kusitishwa,” amesema Shombe na kuongeza kuwa katika uwekezaji huo, mwekezaji atakuwa na asilimia 64 na Serikali 36.
Akimtaja mwekezaji huyo kuwa ni Fujian xho Company Limited ambaye wameingia naye ubia Na kwamba Yuko nchini, ana kiwanda kingine.
Shombe amesema Kwa sasa hivi viwanda vyote vya chuma vinatumia malighafi za chuma chakavu, hivyo kiwanda hicho kitazalisha chuma ghafi ambazo zitatumiwa na viwanda vingine na bidhaa nyingi za chuma zitasaidika na kiwanda hicho.
Amesema ukikamilika utakuwa na faida kubwa, kutoagiza tena bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi, lakini pia Tanzania inaweza kuuza nje ya nchi na kupata fedha za kigeni na kusaidia viwanda kupata malighafi na kuongeza ajira na kusaidia taifa.
.
Akizungumza Jafo ameagiza NDC kuhakikisha miradi yote inafanyiwa kazi na kusimamia taratibu ziweze kukamilika na kupata wawekezaji.
Amesema NDC ni shirika kubwa linategemewa na Taifa hivyo liifanye vizuri Kwa kuwa ni roho ya uchumi.
“Tujue tuna dhana na kubwa ya kutunza rasilimali
Tunahitaji uratibu imara ….tutapambana pamoja kuhakikisha NDC inafanya vizuri tumsaidie Rais,” amesema Jafo.