Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 4

Kasekenya Awapa Pole Waathirika Wa Moto Ileje, Atoa Msaada Wa Matibabu

Na Mwandishi Wetu
ILEJE: MBUNGE wa Ileje ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya, ametoa pole kwa wananchi walioathiriwa na moto ulioteketeza mashamba ya miti wilayani humo, huku akitoa msaada wa fedha za matibabu kwa baadhi ya waathirika.
Kasekenya amewataka wananchi kuendelea kushirikiana kuwapatia waathirika hao hifadhi na huduma za matibabu wakati Serikali ikiendelea na juhudi za kutafuta misaada zaidi kwa ajili yao.
Akiwa katika ziara ya jimboni humo, mbunge huyo amekabidhi misaada mbalimbali, ikiwemo fedha za kugharamia matibabu kwa baadhi ya waathirika, huku akisisitiza umuhimu wa jamii kusaidiana wakati wa majanga.
Habari Picha 14247
Moto huo, unaodaiwa kuzuka Oktoba 23, 2026, umeteketeza mashamba ya miti ya wananchi katika vijiji vya Chilemba, Lali, Shikunga na Ibaba.
Kutokana na athari hizo, wananchi walioathirika wameiomba Serikali kuwapatia miche ya miti ili waweze kuanzisha upya mashamba yao mara mvua zitakapoanza.
Habari Picha 14248
Habari Picha 14249
Habari Picha 14250
Habari Picha 14251
Habari Picha 14252
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.