Mfanyakazi Tanzania ni jukwaa la taarifa linalowakusanyia wafanyakazi habari za ajira, sheria za kazi, haki na wajibu wa mfanyakazi, matangazo rasmi, nyaraka za umma pamoja na fursa za elimu na mafunzo.
WAKALA wa Taifa wa Hifadhi Ya Chakula (NFRA) inaelimisha jamii mbinu mbalimbali za uhifadhi wa chakula ili wakulima waweze kutunza chakula kwa njia zilizo bora pamoja na kukabiliana na mvua za Elnino.
Aidha Wakala umesema ipo njia ya asili ya kutambua mazao yaliyokauka ili yaweze kuhifadhiwa ikiwa ni pamoja na kuweka mazao hayo kwenye chupa kavu ya plastiki na kuchanganya na chumvi kisha kuifunga na inaweza kutoa matokeo baada ya dakika tano.
Ofisa Kilimo kuyoka NFRA Mathay Hhando amesema hayo katika siku ya chakula duniani inayoadgimishwa mkoani Tanga katika viwanja vya Usagara.
Amesema NFRA inawafundisha wakulima kuhifadhi chakula kwa mbinu bora ili kisiharibike na kuwa salama kwa matumizi.
Amesema mkulima anaweza kuhifadhi chakula kwenye mifuko maalum lakini sharti isiwekwe kugusana na sakafu ama ukuta wa nyumba,jambo litakalowezesha mazao kukaa kwa muda mrefu huku akiepuka pia kutumia viuatilifu kuhifadhi mazao.
“Matumizi ya viuatilifu ni gharama na kwa kutumia njia ya asili mkulima anaweza pia kuhifadhi mazao katika kihenge cha bati maalum pale ambapo mazao yanakuwa yamekauka,” amesema.
Kuhusu matumizi ya chumvi na chupa amesema mkulima ataweka robo ya mazao hayo kwenye chupa ya plastiki ambayo ni kavu na kuchanganya na vijiko viwili vya chumvi na kuweka chupa hiyo kwenye kivuli na baadabya dakika tano kama chumvi ndani ya chupa itaonesha kuyeyuka ni wazi kuwa mazao hayajakauka ipasavyo.
Amesema iwapo chumvi haitoyeyuka na kubakia kama ilivyo basi mazao hayo yanakuwanyamekauka na yanahitaji kuhifadhiwa.
“Zipo njia nyingine za kujua kama mazao yamekauka ikiwa ni pamoja na kung’ata punje,kusikiliza mlio wa mazao kwa kumimina kwenye vyombo,” amesema na kuongeza kuwa njia nyingine ya kisasa ninkutumia madhine maalum yankupima unyevu kwenye mazao.
Maoni 0
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!