MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Profesa YANDA:  Tanzania Ihitaji Teknolojia Kufuatilia Uharibifu Wa Mazingira
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Profesa YANDA:  Tanzania Ihitaji Teknolojia Kufuatilia Uharibifu Wa Mazingira
MakalaUncategorized

Profesa YANDA:  Tanzania Ihitaji Teknolojia Kufuatilia Uharibifu Wa Mazingira

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Asema uanachama GGGI utafungua fursa za teknolojia, fedha za miradi ya tabianchi
Na Lucy Ngowi
Dodoma: TANZANIA inahitaji kuwekeza katika teknolojia za kisasa zitakazowezesha Serikali kufuatilia uharibifu wa mazingira nchini kote na kufanya tathmini sahihi ya hewa ukaa (carbon), Profesa Pius Yanda amesema.
Akichangia Azimio la Bunge kuhusu kuridhia uanzishwaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Ukuaji wa Kijani (Global Green Growth Institute-GGGI), Profesa Yanda amesema uanachama wa Tanzania katika taasisi hiyo unaweza kuongeza uwezo wa nchi kupata teknolojia, utaalamu na fursa za fedha kwa ajili ya miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
GGGI ni taasisi ya kimataifa ya kiserikali inayolenga kusaidia nchi zinazoendelea na zinazoibukia kukuza uchumi kwa namna inayolinda mazingira, kupunguza uzalishaji wa hewa chafu na kuongeza ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Pia husaidia nchi kuandaa miradi ya kijani na kuchochea upatikanaji wa uwekezaji na fedha kwa miradi hiyo.
Profesa Yanda amesema Tanzania, kama zilivyo nchi nyingine zinazoendelea, inakabiliwa na athari za mazingira na mabadiliko ya tabianchi, hivyo inahitaji rasilimali, teknolojia na kujengewa uwezo ili kukabiliana na changamoto hizo.
“Katika eneo la tathmini ya hewa ukaa (carbon), tunahitaji teknolojia zaidi,” amesema Profesa Yanda.
Amesema mahitaji hayo yanakuwa muhimu zaidi kutokana na kuongezeka kwa majukumu ya kusimamia mazingira, akisisitiza umuhimu wa Tanzania kuwa na mfumo wa kiteknolojia unaoweza kufuatilia hali ya mazingira katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa ufanisi.
“Tunahitaji kufikia hatua ya kuwa na teknolojia inayoweza kufuatilia uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa ufanisi. Haya yote yanahitaji ushirikiano na taasisi kubwa kama GGGI,” amesema.
Profesa Yanda amesema Serikali tayari imekuwa ikishirikiana na taasisi za kimataifa, zikiwemo UNEP na UNDP, ambazo zimekuwa zikisaidia katika maeneo ya teknolojia, kujenga uwezo na kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
Amesema taasisi hizo huwezesha nchi kupata fedha kupitia mifuko ya kimataifa ya mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo GEF na GCF, huku akieleza kuwa GGGI inaweza kuwa taasisi ya ziada itakayosaidia Tanzania kufikia malengo yake ya maendeleo ya kijani.
Profesa Yanda amesema hatua hiyo inaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ambayo imeweka mazingira na mabadiliko ya tabianchi miongoni mwa maeneo muhimu ya maendeleo ya Tanzania.
Amesema Tanzania ina kila sababu ya kuimarisha ushirikiano na GGGI na kutumia fursa zitakazopatikana, lakini akasisitiza umuhimu wa Serikali kuandaa mapema mawazo na mapendekezo ya miradi yenye ubora ili iweze kunufaika na fursa za fedha na teknolojia.
“Tuna kila sababu sasa ya kuhakikisha kwamba na sisi tunakuwa wanachama ili tuweze kunufaika na taasisi hiyo,” alisema.
Taarifa ya GGGI inaonyesha Tanzania ipo katika hatua ya mchakato wa kujiunga na taasisi hiyo, pamoja na nchi nyingine kadhaa.
Profesa Yanda amehitimisha kwa kuunga mkono Azimio hilo.

You Might Also Like

July 14, 2026

Tanzania yang’ara miradi ya Kinywe

Wanachuoni Katika Mawasilianao ya Utamaduni kati ya China na Afrika

Rais Samia ametekeleza kwa vitendo falsafa ‘kazi iendelee’

SmartDarasa: Tunda la Miaka 40 ya COSTECH Linalobadili Elimu ya Sayansi Tanzania

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ujenzi Sports Club Yatoa Msaada Kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum, Dodoma
Next Article Tanzania Yalenga Kuzalisha, Si Kununua Teknolojia
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tanzania Yalenga Kuzalisha, Si Kununua Teknolojia
Habari September 3, 2026
Ujenzi Sports Club Yatoa Msaada Kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum, Dodoma
Habari September 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuchukua Hatua Kuimarisha Sekta Ya Elimu,Kupanua Fursa Za Elimu Ya Sekondari
Habari September 3, 2026
Serikali Yachunguza Sheria Mpya Ya Biashara Mtandao
Habari September 3, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?