MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yachunguza Sheria Mpya Ya Biashara Mtandao
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yachunguza Sheria Mpya Ya Biashara Mtandao
Habari

Serikali Yachunguza Sheria Mpya Ya Biashara Mtandao

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Yataka Mapengo YA Sheria Yaliyopo Yabainishwe

Na Lucy Ngowi

SERIKALI imeagiza kufanyika kwa utafiti wa kina kuhusu umuhimu wa kutungwa kwa Sheria mahsusi ya Biashara Mtandao (E-Commerce Law), ikiwa ni hatua ya kukabiliana na changamoto za kisheria zinazojitokeza kutokana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, ametoa agizo hilo katika kikao na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, George  Mandepo, kilichojadili maboresho ya sheria yanayolenga kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Habari Picha 13568

Katika kikao hicho, viongozi hao walitathmini namna mabadiliko ya teknolojia na ongezeko la matumizi ya majukwaa ya kidijitali katika kufanya biashara yanavyohitaji mfumo wa sheria unaokwenda sambamba na mazingira hayo.

Kwa mujibu wa maelekezo hayo, utafiti utapitia sheria zilizopo ili kubaini mapengo na changamoto za kisheria zinazohusiana na biashara mtandao, pamoja na kufanya ulinganisho na mifumo ya sheria inayotumika katika nchi nyingine.

Miongoni mwa maeneo yatakayochunguzwa ni mikataba ya kielektroniki, ulinzi wa watumiaji, uendeshaji wa majukwaa ya kidijitali, malipo ya kielektroniki na ulinzi wa taarifa binafsi.

Pia, utafiti huo utazingatia usalama wa miamala ya kielektroniki, haki miliki, masuala ya kodi, ushindani na namna ya kutatua migogoro inayotokana na biashara zinazofanyika mtandaoni.

Biashara mtandao imeendelea kuwa sehemu muhimu ya shughuli za kiuchumi, ikirahisisha uuzaji wa bidhaa na huduma kupitia teknolojia za kidijitali katika sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo.

Waziri Homera ameitaka Tume ya Kurekebisha Sheria kuanzisha utafiti huo na kuandaa mapendekezo yatakayowezesha Serikali kuamua iwapo kuna haja ya kutungwa kwa Sheria mahsusi ya Biashara Mtandao au kufanyiwa maboresho sheria zilizopo.

Serikali inaona hatua hiyo kuwa muhimu katika kujenga mazingira salama na rafiki kwa wafanyabiashara na watumiaji wa huduma za kidijitali, huku ikichochea ubunifu, ushindani na uwekezaji katika uchumi wa kidijitali.

Aidha, matokeo ya utafiti yanatarajiwa kusaidia Tanzania kutumia kikamilifu fursa zinazotokana na uchumi wa kidijitali na kuimarisha ulinzi wa maslahi ya wafanyabiashara na watumiaji.

You Might Also Like

UDSM  Yakamilisha Utafiti Wa Dawa Ya Kusafisha Sumu Kwenye Maji

Profesa Mutembei apongeza serikali kuruhusu mchepuo lugha ya kichina

Tanzania Yafungua Milango Ya Biashara Na Jumuiya Ya Ulaya

Rais TUCTA Apongeza Mfuko Wa NSSF Kwa Ongezeko La Thamani Hadi Trilioni 9

Sirro: Kasulu Itambue Thamani ya Uwekezaji, Itenge Maeneo Rasmi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Zhou Enlai na Julius Nyerere: Urafiki Uliovuka Mipaka Milima, Bahari
Next Article Serikali Yaendelea Kuchukua Hatua Kuimarisha Sekta Ya Elimu,Kupanua Fursa Za Elimu Ya Sekondari
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Yaendelea Kuchukua Hatua Kuimarisha Sekta Ya Elimu,Kupanua Fursa Za Elimu Ya Sekondari
Habari September 3, 2026
Zhou Enlai na Julius Nyerere: Urafiki Uliovuka Mipaka Milima, Bahari
Makala September 2, 2026
TANESCO Yabaini Matukio Ya Wizi Wa Umeme Kinondoni Kaskazini
Habari September 2, 2026
MOI Yafanikiwa Kupunguza Rufaa Za  Wagonjwa Wa Mifupa Kwa Asilimia 98
Habari September 1, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?