MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania Yalenga Kuzalisha, Si Kununua Teknolojia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania Yalenga Kuzalisha, Si Kununua Teknolojia
Habari

Tanzania Yalenga Kuzalisha, Si Kununua Teknolojia

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Korea Kusini yafungua fursa za utafiti, ubunifu, uhamishaji teknolojia na ajira kwa Watanzania
Na Mwandishi Wetu,
Incheon, Korea Kusini: TANZANIA iko mbioni kupata fursa mpya za utafiti, ubunifu, uhamishaji wa teknolojia na ajira za kisasa baada ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Kongani ya Ubunifu ya Incheon (IIC) kuweka msingi wa kuanzisha tawi la IIC nchini.
Ushirikiano huo unalenga kuwaunganisha watafiti, wabunifu na wataalamu wa Tanzania na mfumo wa ubunifu wa Korea Kusini, hatua inayotarajiwa kuongeza uwezo wa Watanzania kuendeleza teknolojia kutoka hatua ya utafiti hadi matumizi ya kibiashara.
Hatua hiyo imeainishwa Septemba 3, 2026, wakati wa hafla ya IIC Global Branch MOU Ceremony iliyofanyika Songdo Convensia, Incheon, Korea Kusini, sambamba na Mkutano wa Kimataifa wa Teknolojia za Mazingira wa Incheon 2026.
Habari Picha 13599
Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Noel Kaganda, amesema ushirikiano huo unapaswa kujenga uwezo wa pande zote badala ya Tanzania kubaki mtumiaji wa teknolojia zinazozalishwa na wengine.
“Ubunifu lazima uwe shirikishi. Hatupaswi kuwa na nchi moja inayozalisha na nyingine inayobaki kuwa mtumiaji pekee katika ikolojia ya ubunifu,” amesema.
Amesema Tanzania inapaswa kutumia fursa hiyo kujenga mazingira yatakayowawezesha wataalamu wake kushiriki katika kubuni, kuendeleza na kujaribu teknolojia zinazokidhi mahitaji ya nchi.
Habari Picha 13600
Makubaliano hayo yameainisha ushirikiano katika utafiti wa pamoja, maendeleo ya teknolojia na ubunifu, uhamishaji wa teknolojia, ubia wa kibiashara pamoja na shughuli za kitaaluma na kitaalamu.
Kwa vijana na wataalamu, ushirikiano huo unaweza kufungua nafasi za kupata ujuzi kupitia miradi ya pamoja na taasisi za utafiti, kampuni na wataalamu wa Korea Kusini, huku ukiongeza uwezekano wa bunifu za Kitanzania kufikia soko na kuanzisha biashara.
Aidha, makubaliano hayo yametoa nafasi ya kuandaa ramani ya kimkakati kuelekea kuanzishwa kwa Kituo cha Sayansi na Teknolojia cha K-Africa.
Balozi Kaganda amesema ushirikiano huo ni sehemu ya diplomasia ya sayansi, teknolojia na ubunifu na kuitaka COSTECH na IIC kuhakikisha makubaliano hayo yanazaa matokeo yenye tija.
Hatua hiyo imeendana na msisitizo wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, aliyehimiza Tanzania kujifunza uzoefu wa Korea Kusini katika kutumia sayansi, teknolojia na ubunifu kuchochea maendeleo ya uchumi.

You Might Also Like

TRAWU Kupambania Mkataba Wa Hali Bora Kwa Wafanyakazi

TDB Yaheshimisha Tasnia Ya Maziwa

Brela Yatoa Huduma Zote Za Usajili Katika Maonesho Ya Teknolojia Ya Madini Geita

Mikataba ya zaidi ya bilioni 50 kuhamasisha nishati salama

JOWUTA Yawasilisha Ripoti ya Ukaguzi kwa Msajili

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Profesa YANDA:  Tanzania Ihitaji Teknolojia Kufuatilia Uharibifu Wa Mazingira
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Profesa YANDA:  Tanzania Ihitaji Teknolojia Kufuatilia Uharibifu Wa Mazingira
Makala Uncategorized September 3, 2026
Ujenzi Sports Club Yatoa Msaada Kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum, Dodoma
Habari September 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuchukua Hatua Kuimarisha Sekta Ya Elimu,Kupanua Fursa Za Elimu Ya Sekondari
Habari September 3, 2026
Serikali Yachunguza Sheria Mpya Ya Biashara Mtandao
Habari September 3, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?