Na Lucy Lyatuu,Dodoma
KATIKA Kuadhimisha siku ya vijana duniani,vijana wametakiwa kutambua kuwa fursa zipo lakini waangalie zile zilizoko ndani ya uwezo wao wakianzia pale walipo.
Ofisa mradi wa Tuinuke Pamoja unaotekelezwa na Aghakan Foundation na kufadhiliwa na serikali ya Ireland,Eric Kisiga amesema hayo wakati akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Amesema kupitia mradi huo unatekelezwa katika mkoa wa Dodoma kwenye wilaya sita za Kondoa,Chamwino, Chemba,Bahi, ukilenga kuleta usawa wa kijinsia kuweza kufikia makundi mbalimbali ya vijana na wenye ulemavu ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiachwa na fursa.

” Leo siku ya vijana tumeshirikisha vijana katika mradi wa Tuinuke Pamoja na vijana 25 wameshikiriki hata katika mijadala mnalimbali,” amesema na kuongeza kuwa pia wameleta bidhaa wanazozalisha kama kikundi na kuelezea shughuli zao wanazofanya.
Amesema kupitia kauli mbiu ya maonesho kuwa Mazingira Tofauti Fursa Sawa kwa wote inahimiza ushirikishwaji wa vijana katika maeneo mbalimbali bila kujali tofauti zao na za maeneo waliyopo,elimu waliyonayo bali wanapaswa haki sawa kwenye nyanja mnalimbali zikiwemo za uchumi.
“Mchango wao na.mawazo waliyoyatoa leo katika maadhimisho ya siku ya vijana yamekabidhiwankwa Waziri wa Maendelei ya Vijana, Joel Nanauka ambayo yatasaidia kutengeneza sera jumuishi ya vijana,”amesema.
Kuhusu vijana amewataka kuanzia walipo na kuhakikisha wanatekeleza mipango yao kwa vitendo kama wanavyoipanga kwa kuwa wengi hushindwa.
Amesema katika maadhimisho haho vijana wameweza kutengeneza mitandaonya mawasiliano,wakibadilishana ujuzi na kuelezana uzoefu kulingana na maeneo waliyopo.




