MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mabilika Kutoka Ubunifu Hadi Soko La Afrika
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Mabilika Kutoka Ubunifu Hadi Soko La Afrika
Makala

Mabilika Kutoka Ubunifu Hadi Soko La Afrika

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
9 Min Read
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu akifurahia jambo na mbunifu Innocent Mabilika katika Maonesho ya Nanenane yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dodoma.
Na Lucy Ngowi
AKIWA na umri wa miaka 26, Innocent Mabilika amefika hatua ambayo ubunifu wake hauishii tena kwenye karakana.
Mashine anazotengeneza zinatumika na wakulima na wafanyabiashara, zimeanza kuuzwa nje ya Tanzania na zimekuwa chanzo cha ajira na mafunzo kwa vijana.
Lakini nyuma ya mafanikio hayo kuna changamoto inayoweza kuamua hatua inayofuata ya safari yake, uwezo wa uzalishaji hauendani na mahitaji ya soko.
Mabilika, mwanzilishi wa Machinery Innovations Limited, anasema hadi sasa ametengeneza zaidi ya mashine 150, huku mwaka huu 2026 pekee akiwa ameuza takribani mashine 68.
Mashine hizo ni pamoja na za kulimia, kupanda, kupalilia na kuvuna, pamoja na mashine za kutotolesha mayai na nyingine zinazolenga kurahisisha shughuli za kilimo na kuongeza tija.
“Kwa mwaka huu 2026 nimeuza mashine 68. Wateja wengi nimewapata Iringa, Njombe, Morogoro na Mbeya. Hata sasa nina mashine zinazokwenda Kilosa,” anasema.
Akizungumza katika Viwanja vya Nzuguni,  Nanenane jijini Dodoma, anasema
Safari yake ilianza mwaka 2014 akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi,  Wakati huo hakuwa na karakana wala mitambo ya kisasa.
Habari Picha 13203
Anasema Alianza kutengeneza vitu kwa udongo, baadaye plastiki, kabla ya kuingia kwenye kazi za chuma baada ya kumaliza kidato cha nne.
Kipaji hicho kilichoanza kama shauku ya mtoto kilibadilika kuwa ujuzi wa kutengeneza zana na mashine zilizolenga kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.
Leo, bidhaa zake zinahusisha mashine za kulimia, kupanda, kupalilia na kuvuna, huku baadhi zikitumika pia katika shughuli nyingine za uzalishaji.
Miongoni mwa bidhaa zake ni matrekta madogo yanayouzwa kwa kati ya Sh. Milioni nane na Sh. Milioni 12, kulingana na aina na mahitaji ya mteja.
Soko la Mabilika halijaishia Tanzania.
Anasema baadhi ya mashine zake zimefika Msumbiji, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Ameshauza mashine mbili Msumbiji, moja DRC na nyingine Zambia, huku akiwa amesaini mkataba wa kutengeneza zaidi ya mashine 10 kwa mteja mmoja wa nje ya nchi.
Kwa Mabilika, soko hilo linaonyesha kuwa teknolojia inayotengenezwa na Mtanzania inaweza kuvuka mipaka iwapo itapata uwezo wa kuzalishwa kwa kiwango kinachohitajika.
Tatizo si ubunifu, ni uzalishaji
Ukuaji wa soko umeleta changamoto nyingine. Mabilika anasema tatizo lake kubwa kwa sasa si kukosa mawazo au uwezo wa kutengeneza mashine, bali ukosefu wa mitambo ya kisasa inayoweza kuongeza kasi na usahihi wa uzalishaji.
Anahitaji mitambo ikiwamo CNC na sheet bending machine, pamoja na mashine nyingine za kukata, kuchonga, kutoboa na kuchomelea chuma.
CNC humwezesha kuchakata vipande vya chuma kwa usahihi kulingana na michoro ya kompyuta, wakati sheet bending machine hutumika kukunja mabati na vipande vya chuma kwa vipimo maalumu.
Habari Picha 13206

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye, akiwa na mbunifu Innocent Mabilika mbele ya mashine ya kumenya viazi mviringo iliyotengenezwa na mbunifu huyo.

“Changamoto yangu kubwa kwa sasa ni mitambo na zana bora za uzalishaji. Sina mitambo ambayo itanisaidia kuongeza uzalishaji. Badala ya kuzalisha mashine nne au tano kwa mwezi, wakati mwingine najikuta nazalisha mbili,” anasema.
Anasena, kwa sasa anaweza kuzalisha takribani mashine nne kubwa kwa mwezi, huku mashine ndogo zikifikia takribani 10.
Akifanikiwa kupata mitambo hiyo, anaamini anaweza kuongeza uzalishaji wa mashine kubwa hadi takribani nane kwa mwezi.
Hivyo, anachohitaji si fedha pekee. Yuko tayari hata kuunganishwa na mwekezaji atakayesaidia kuwekeza kwenye mitambo hiyo ili kuongeza uzalishaji.
“Sitaki lazima nipewe mtaji. Ningependa hata nipate mitambo au mwekezaji awekeze kwenye mitambo. Mimi nifanye kazi na alipwe fedha yake,” anasema.
Baraka Honda, mfanyabiashara aliyenunua mashine ya Mabilika kwa ajili ya kuvunja mahindi yanayotumika kutengeneza chakula cha kuku, anasema mashine hiyo imemsaidia kuongeza ufanisi.
“Gunia moja la mahindi linaweza kuvunjwa kwa dakika 10, kutegemea ukubwa wa mashine,” anasema.
Mbali na kutengeneza mashine, Mabilika ameanza kujenga kizazi cha vijana wenye ujuzi wa vitendo.
Anasema amewafundisha vijana 16 katika kazi mbalimbali zinazohusiana na uzalishaji wa mashine.
Kati yao, vijana wanne wana ajira za kudumu, wakiwamo wawili wanaoshughulikia masoko na wengine wanaofanya kazi za kiufundi.
Habari Picha 13205
Vijana wengine wanaendelea kupata mafunzo ya vitendo kabla ya kuingia kwenye ajira rasmi.
“Napokea kijana yeyote anayetamani kujifunza ninachokifanya. Hata kama maisha ni magumu, akitamani kujifunza, niko tayari kumsaidia,” anasema.
COSTECH: Kuunganisha ujuzi na elimu
Hata hivyo, kadiri teknolojia inavyobadilika, Mabilika amegundua kuwa ujuzi wa vitendo pekee hautoshi. Hapo ndipo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ilipoingia katika safari yake.
Mabilika alipata fursa ya kuongeza elimu yake ya ufundi baada ya COSTECH kutambua uwezo aliouonyesha kupitia ubunifu na kazi za vitendo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt.Amos Nungu, Mabilika aliwasilisha ombi la kupata fursa ya kuongeza ujuzi wake.
Ombi hilo lilifuatwa na maelekezo ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, kwamba apelekwe katika taasisi ya elimu kwa ajili ya mafunzo maalumu.
Hatua ambayo inampa nafasi ya kuunganisha ujuzi alioupata kwa vitendo na elimu ya kitaalamu.
Kwa Mabilika, elimu hiyo ni muhimu kwa sababu teknolojia anazokutana nazo katika utengenezaji wa mashine zinahitaji uelewa wa kompyuta, programu na mifumo ya sensa.
“Imenisaidia kunipa elimu na kunifanya nitamani kuendeleza ubunifu wangu katika uhalisia wa masomo ili nifanye vizuri zaidi,” anasema.
Kwa maana hiyo, hatua ya COSTECH haikufuta ujuzi aliokuwa nao Mabilika, inausaidia kuunganisha ujuzi wa mikono na elimu ya kitaalamu.
Baada ya kujenga uwezo wa kubuni, kutengeneza, kuuza na kuwafundisha vijana, Mabilika sasa anakabiliwa na hatua nyingine ya ukuaji, kuongeza uwezo wa uzalishaji.
Akipata CNC, mashine ya kukunja mabati na mitambo mingine anayohitaji, anaamini ataweza kupunguza muda wa uzalishaji, kuongeza idadi ya mashine, kuhudumia oda nyingi zaidi na kuongeza ajira.
Kwa mtazamo huo, ombi lake la mitambo si suala la kuongeza vifaa kwenye karakana pekee. Ni hitaji la kuongeza uwezo wa teknolojia inayotengenezwa nchini ili iweze kukidhi soko linaloanza kuonekana ndani na nje ya Tanzania.
Mabilika anaamini Serikali ikiweka mazingira bora kwa wabunifu wa ndani, Tanzania inaweza kupunguza utegemezi wa baadhi ya mashine na zana kutoka nje.
“Badala ya Serikali kuagiza mashine na zana mbalimbali kutoka nje, iwekeze kwenye ubunifu wa Watanzania ili tuweze kufanya biashara kwa mapana zaidi,” anasisitiza.
Safari ya Mabilika inaweka sura halisi katika mjadala wa miaka 40 ya COSTECH.
Inaonyesha kuwa kukuza sayansi, teknolojia na ubunifu hakumaliziki kwa kumtambua mbunifu. Kunahitaji pia elimu, miundombinu, mitambo, soko na mazingira yatakayomwezesha mbunifu kubadili wazo kuwa bidhaa yenye thamani.
Mabilika tayari ameonyesha matokeo kwa
Kutengeneza zaidi ya mashine 150, ameuzia wateja takribani mashine 68 mwaka 2026, amefikisha bidhaa zake katika nchi jirani, ameajiri vijana na amekuwa akiwafundisha wengine.
Kinachomzuia sasa si ukosefu wa wazo, bali uwezo wa kulitekeleza kwa kiwango kikubwa.
Safari iliyoanza kwa udongo mwaka 2014 sasa imefika kwenye chuma, teknolojia na soko la kikanda.
Hatua inayofuata ni kuvuka kutoka karakana inayotegemea nguvu za mikono kwenda uzalishaji unaotumia mitambo ya kisasa.
Hapo ndipo simulizi ya Mabilika inakuwa zaidi ya hadithi ya kijana mbunifu. Inakuwa mfano wa namna kipaji kinavyoweza kugeuka kuwa ujuzi, ujuzi kuwa teknolojia, teknolojia kuwa biashara, na biashara kuwa ajira na bidhaa inayoweza kufika katika soko la Afrika.
Habari Picha 13204

 

You Might Also Like

BAADHI YA MATUKIO MAKUBWA YA UKATILI YALIYOFANYIKA MWAKA 2024

OSHA yaelimisha sheria mahala pa kazi kwa JOWUTA

Ukarabati wa Reli Ya TAZARA Wafungua Ukurasa Mpya China, Afrika

Shen Zhiying: Mkongwe Aliyeanzisha Kozi Ya Kiswahili Nchini China

Kiswahili Chavuka Mipaka, Paris Yajiandaa Kukipokea

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TARURA Yafungua Njia Mpya Kukwepa Msongamano Dodoma
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TARURA Yafungua Njia Mpya Kukwepa Msongamano Dodoma
Habari August 9, 2026
TPHPA Kuja Na Ramani Ya Visumbufu Nchi Nzima
Habari August 9, 2026
Dkt. Samia: Ushirika Simamieni Matrekta Kwa Manufaa Ya Wakulima
Habari August 9, 2026
Jeshi La Zimamoto Yaimarisha Elimu Kwa Wananchi Kuhusu Matumizi Salama Ya Nishati Ya Kupikia
Habari August 9, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?