MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TARURA Yafungua Njia Mpya Kukwepa Msongamano Dodoma
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TARURA Yafungua Njia Mpya Kukwepa Msongamano Dodoma
Habari

TARURA Yafungua Njia Mpya Kukwepa Msongamano Dodoma

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAKATI ongezeko la shughuli za Serikali, biashara na ujenzi likiendelea kuongeza msongamano wa magari Dodoma, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeanza kupanua mtandao wa barabara ili kufungua njia mbadala za usafiri na kurahisisha uunganishaji wa maeneo mbalimbali ya mji.
Mhandisi wa TARURA Mkoa wa Dodoma, Revocatus Daniel Nsubile, amesema hayo katika maonesho ya nane nane yaliyomalizika na kuongeza,  maboresho hayo yanalenga kuimarisha mawasiliano kati ya Dodoma mjini na maeneo muhimu, ikiwamo Chamwino ambako kuna Mji wa Serikali na taasisi mbalimbali.
Amesema uboreshaji wa barabara hizo utawapa wananchi njia mbadala za usafiri na kusaidia kupunguza utegemezi wa barabara zinazotumika kwa wingi, hatua inayotarajiwa kurahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi.
“Tunapoendelea kuboresha barabara hizi, tunalenga kuwasaidia wananchi kufika maeneo yao kwa urahisi na pia kupunguza msongamano katika barabara zinazotumika kwa wingi,” amesema.
Nsubile amesema TARURA Mkoa wa Dodoma unasimamia mtandao wa barabara katika wilaya saba za mkoa huo, huku ujenzi, ukarabati na matengenezo ukiendelea.
Amesema kwa mwaka wa fedha 2026/27, TARURA imeanza mchakato wa utekelezaji wa miradi mipya, ikiwamo uboreshaji wa barabara zinazolenga kuongeza ufanisi wa usafiri.
Amesema barabara bora pia zitasaidia wakulima kusafirisha mazao kutoka maeneo ya uzalishaji kwenda masokoni kwa urahisi.
Aidha, amewataka wananchi kulinda miundombinu ya barabara, ikiwamo taa na alama, na kutoa taarifa za wizi au uharibifu kwa viongozi na vyombo vya ulinzi na usalama.

You Might Also Like

Mwanachama Wa TALGWU Akutwa Hana Hatia

IITA Yawekeza Bilioni 410 Tanzania Kuimarisha Kilimo, Utafiti

Mkandarasi Atakiwa Kukamilisha Mradi Kwa Wakati

COSTECH Yasaini Mkataba Ujenzi Jengo La Sayansi, Teknolojia, Ubunifu

SELF Yahamasisha Wananchi Kunufaika na Mikopo Nafuu ya Maendeleo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TPHPA Kuja Na Ramani Ya Visumbufu Nchi Nzima
Next Article Mabilika Kutoka Ubunifu Hadi Soko La Afrika
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mabilika Kutoka Ubunifu Hadi Soko La Afrika
Makala August 9, 2026
TPHPA Kuja Na Ramani Ya Visumbufu Nchi Nzima
Habari August 9, 2026
Dkt. Samia: Ushirika Simamieni Matrekta Kwa Manufaa Ya Wakulima
Habari August 9, 2026
Jeshi La Zimamoto Yaimarisha Elimu Kwa Wananchi Kuhusu Matumizi Salama Ya Nishati Ya Kupikia
Habari August 9, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?