MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt. Samia: Ushirika Simamieni Matrekta Kwa Manufaa Ya Wakulima
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt. Samia: Ushirika Simamieni Matrekta Kwa Manufaa Ya Wakulima
Habari

Dkt. Samia: Ushirika Simamieni Matrekta Kwa Manufaa Ya Wakulima

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeamua kutumia Vyama vya Ushirika kama nguzo muhimu katika usimamizi na utoaji wa huduma za zana za kilimo kwa wakulima nchini, akieleza kuwa taasisi hizo ziko karibu na wakulima na zinaelewa mahitaji yao.
Rais Samia amesema uamuzi huo unalenga kuhakikisha matrekta na zana nyingine za kilimo zitakazokabidhiwa kwa Vyama vya Ushirika zinatumika ipasavyo kuongeza tija, uzalishaji na kipato cha wakulima katika maeneo yao.
Akizungumza  hayo wakati wa hafla ya kukabidhi vitendea kazi kwa Wakala wa Taifa wa Huduma za Ugani (NAESA) na Vyama vya Ushirika, Rais Samia amesema Serikali awali ilikuwa na mpango wa kuanzisha vituo vya zana za kilimo katika Kanda mbalimbali nchini.
Habari Picha 13185
Hata hivyo, amesema baada ya kutafakari namna bora ya kuwafikishia wakulima huduma hizo, Serikali imeona Vyama vya Ushirika vina nafasi kubwa zaidi kutokana na kuwa karibu na wakulima.
“Sasa tunaanza na nyie, nitakabidhi matrekta yaliyopo hapa yaende yakafanye kazi. Tutaendelea kununua hadi tueneze kama tulivyoahidi,” amesema.
Amesema Vyama vya Ushirika vitakuwa na jukumu la kusimamia matrekta hayo na kuhakikisha yanawafikia wakulima wanaohitaji huduma za zana za kilimo kwa wakati.
“Tumewakabidhi matrekta haya na zana tutakazonunua kwa Vyama vya Ushirika ili wao wawasimamie wakulima wao,” amesema.
Rais Samia amesisitiza kuwa matrekta na zana hizo hazipaswi kutumika kinyume na malengo yaliyokusudiwa, bali ziendelee kuwa sehemu ya juhudi za Serikali kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji.
Amesema Serikali itaendelea kununua na kukabidhi matrekta pamoja na zana nyingine za kilimo kwa Vyama vya Ushirika katika Kanda mbalimbali, hatua inayolenga kupunguza changamoto ya upatikanaji wa zana na kuongeza tija katika kilimo.
Kwa mujibu wa Rais Samia, mfumo huo utaiwezesha Serikali kuwafikia wakulima kwa ufanisi zaidi kupitia Vyama vya Ushirika, huku vyama hivyo vikitakiwa kuhakikisha vifaa vinavyokabidhiwa vinawanufaisha wakulima na kuchochea maendeleo ya kilimo katika maeneo yao.
Habari Picha 13187

You Might Also Like

Rais Samia Amkabidhi Tuzo Profesa Ndunguru kwa Kuinua Mapato, Maboresho TPHPA

Luswetula Aagiza Udhibiti Mkali wa Mikopo Kandamizi

TEA, Wizara ya Elimu Zanzibar Kushirikiana Kuimarisha Miradi ya Elimu

Ruhuka: Mdudu Anayetishia Zao la Kahawa, TARI Yaja na Suluhisho

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Jeshi La Zimamoto Yaimarisha Elimu Kwa Wananchi Kuhusu Matumizi Salama Ya Nishati Ya Kupikia
Next Article TPHPA Kuja Na Ramani Ya Visumbufu Nchi Nzima
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TPHPA Kuja Na Ramani Ya Visumbufu Nchi Nzima
Habari August 9, 2026
Jeshi La Zimamoto Yaimarisha Elimu Kwa Wananchi Kuhusu Matumizi Salama Ya Nishati Ya Kupikia
Habari August 9, 2026
DC Kondoa  Aipongeza TFS Kwa Teknolojia Ya Uhifadhi Wa Misitu Na Utali
Habari August 8, 2026
Waziri Nanauka Aipongeza   TARURA Kwa Mpango Wa  CBRM ‎
Habari August 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?