MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: PURA Yawataka Watanzania Kujenga Uwezo Kunufaika Na Sekta Ya Mafuta Na Gesi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > PURA Yawataka Watanzania Kujenga Uwezo Kunufaika Na Sekta Ya Mafuta Na Gesi
Habari

PURA Yawataka Watanzania Kujenga Uwezo Kunufaika Na Sekta Ya Mafuta Na Gesi

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Dodoma
 MAMLAKA  Ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA),  inahamasisha vijana kujenga ujuzi unaohitajika katika sekta ya mafuta na gesi, na kuvitaka vyuo mbalimbali vikuu  kujumuisha masomo yanayohusiana na sekta hiyo katika mitaala yao.
Mkurugenzi Mkuu  wa PURA, Charles Sangweni amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la PURA katika maonesho ya kilimo Nanenane jijini Dodoma.
Amesema ushiriki wa mamlaka hiyo katika Maonesho ya Nane Nane  unalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu shughuli za mkondo wa juu wa sekta ya mafuta na gesi pamoja na fursa zinazopatikana katika sekta hiyo.
Amesema  Serikali inaendelea kushirikisha taasisi za elimu ya ufundi, ikiwemo VETA, ili kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi wanaoweza kushiriki katika shughuli za sekta hiyo.
Sangweni amesema mamlaka hiyo pia inahakikisha wazawa wanashiriki kikamilifu kupitia ajira, utoaji wa huduma na usambazaji wa bidhaa katika shughuli za mafuta na gesi.
Hata hivyo, amesema bado kuna changamoto ya upatikanaji wa wataalamu wenye ujuzi wa juu na baadhi ya bidhaa zinazohitajika na wawekezaji, hali inayosababisha kutegemea wataalamu na bidhaa kutoka nje ya nchi.
Amesema  Tanzania ina maeneo yenye viashiria vya uwepo wa mafuta na gesi asilia, huku tafiti za kijiolojia na tafsiri za data zilizofanyika hadi sasa zikifunika takribani asilimia 30 ya maeneo yanayoaminika kuwa na rasilimali hizo.
Amesema PURA, iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Petroli ya mwaka 2015, ina jukumu la kusimamia na kudhibiti shughuli za mkondo wa juu wa petroli, kutoa ushauri kwa Serikali, kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa, kuongeza manufaa ya rasilimali kwa Taifa, pamoja na kusimamia usalama na ulinzi wa mazingira.
Amesema PURA inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, ikiwemo kusimamia miradi ya kimkakati katika sekta ya gesi. Miongoni mwa miradi hiyo ni mpango wa kuchakata gesi asilia na kuibadilisha kuwa kimiminika (LNG), unaotarajiwa kujengwa mkoani Lindi kwa lengo la kuiwezesha Tanzania kushiriki zaidi katika soko la kimataifa la gesi.

You Might Also Like

TEA Yawaalika Wananchi Kujifunza SDF Unavyofanya Kazi

Heshima ya Udaktari Ni Mwito wa Kulitumikia Taifa: Dkt Ikomba

Miaka Minne Ya Samia Na Sekta Ya Elimu

Rais Samia awasili Zimbabwe

Rais Samia Aipa Neema Miradi Ya Kuzalisha Umeme Iringa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article COSTECH Yapambania Haki Za Wabunifu, Yalenga Kupeleka Bunifu Sokoni
Next Article Waziri Nanauka Aipongeza   TARURA Kwa Mpango Wa  CBRM ‎
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

DC Kondoa  Aipongeza TFS Kwa Teknolojia Ya Uhifadhi Wa Misitu Na Utali
Habari August 8, 2026
Waziri Nanauka Aipongeza   TARURA Kwa Mpango Wa  CBRM ‎
Habari August 8, 2026
COSTECH Yapambania Haki Za Wabunifu, Yalenga Kupeleka Bunifu Sokoni
Habari August 8, 2026
Miaka 40 ya Costech: Ruzuku ya Ubunifu Imegeuza Wazo Kuwa Kiwanda Cha Kimataifa
Makala August 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?