MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Halmashauri Ya Jiji La Dodoma Lawataka Wakulima Kutumia Nanenane Kujifunza Kilimo Cha Kisasa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Halmashauri Ya Jiji La Dodoma Lawataka Wakulima Kutumia Nanenane Kujifunza Kilimo Cha Kisasa
Habari

Halmashauri Ya Jiji La Dodoma Lawataka Wakulima Kutumia Nanenane Kujifunza Kilimo Cha Kisasa

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Dodoma
HALMASHAURI Ya Jiji La Dodoma limewataka wakulima  na wananchi kutumia Maonesho ya Nane Nane kujifunza teknolojia za kisasa za uzalishaji wa mazao, ikiwemo kilimo cha mbogamboga na maua, ili kuongeza tija na kujenga fursa za kiuchumi kupitia kilimo.
Akizungumza katika kitalu cha mbogamboga,maua na miti ya matunda katika viwanja vya  Maonesho ya Nane Nane, Mtaalamu wa Kilimo anayesimamia Sekta ya Mazao katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Agnes Loiso amesema maonesho hayo ni fursa muhimu kwa wakulima kupata elimu ya vitendo kuhusu uzalishaji wa mazao mbalimbali kwa kutumia teknolojia zinazoweza kuongeza tija.
Habari Picha 12982
Habari Picha 12983
Amesema katika maonesho hayo, wakulima watafundishwa namna ya kuzalisha mboga za aina mbalimbali pamoja na maua, ambayo yameanza kuwa fursa ya biashara na ujasiriamali kwa wananchi.
“Wakulima wanashauriwa kujihusisha na uzalishaji wa maua kama wajasiriamali kwa sababu nao ni biashara inayoweza kuwa chanzo cha kipato,” amesema.
Amesema Halmashauri ya Jiji la Dodoma pia imefanya majaribio ya baadhi ya mazao, ikiwemo mapera na zabibu, ambayo yameonyesha matokeo mazuri na baadhi yako tayari yameanza kuzaa matunda.
Habari Picha 12984
Habari Picha 12985
Ameongeza kuwa changamoto zilizojitokeza katika uzalishaji wa baadhi ya mazao zilitokana zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa, hususan kwa mazao yanayohitaji baridi kali.
“Hali ya hewa ilitusumbua kidogo kwenye baadhi ya mazao ambayo yanahitaji baridi kali, lakini mwisho wa siku yalitoa maua japokuwa hayakuwa makubwa sana,” amesema.
Aidha amewataka wananchi wenye maeneo madogo au ambao wamejenga nyumba na kuweka matofali chini kutokata tamaa ya kujihusisha na kilimo, akisema teknolojia za bustani za nyumbani zinaweza kuwa suluhisho.
Amesema wananchi wanaweza kujifunza namna ya kuzalisha mbogamboga katika maeneo madogo yaliyopo nyumbani na kupata chakula kwa matumizi ya familia pamoja na ziada ya kuuza.
Habari Picha 12986
Habari Picha 12987
“Unaweza ukazalisha mboga hata kama huna eneo kubwa la kilimo. Waje wajifunze, wajionee wenyewe na waende wakajaribishe majumbani mwao,” amesema.
Kuhusu dhana kuwa Jiji la Dodoma ni kame nanhalifainkwa kilimo  amesema eneo hilo lina uwezo wa kuzalisha mazao mbalimbali kutokana na uwepo wa maji chini ya ardhi.
Amesema katika maeneo mbalimbali ya Dodoma, maji yanaweza kupatikana kwa kuchimba visima kwa kina kifupi, jambo linalowapa wakulima fursa ya kufanya kilimo cha umwagiliaji.
“Dodoma siyo kame kama wananchi wanavyosema. Maji yapo mengi chini ya ardhi na katika baadhi ya maeneo ukichimba mita chache unakutana na maji,” amesema.
Amesema hali hiyo imewezesha majaribio ya mazao mbalimbali kufanyika na kuonyesha matokeo mazuri, ikiwemo ngano, karoti, vitunguu  viazi, mbaazi,uwele na ufuta huku akisisitiza kuwa wakulima wanaweza kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji na kipato.
Habari Picha 12988
Habari Picha 12989
Ameeleza kuwa Maonesho ya Nane Nane yanatoa nafasi kwa wananchi kuona kwa vitendo teknolojia na mbinu mbalimbali za kilimo, hivyo kuwataka wakulima kutoka maeneo mbalimbali kufika na kujifunza namna bora ya kuongeza tija katika uzalishaji.

You Might Also Like

Rais Samia ashuhudia JOWUTA Ikiwa mwanachama wa  TUCTA 

UVCCM Yazindua Kampeni Ya Kutetea Ukweli, kutokomesha Upotoshaji, Uongo

Askari wa Jeshi La Uhifadhi Kusini Wakumbushwa Wajibu

Majukwaa YA Dini Yaimarishe Mapambano Dhidi ya Magonjwa Ya Mlipuko

NHIF: Ruksa wanachama kutumia NIDA

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Dkt. Nchemba: TPHPA Yazidi Kuwafikia Wakulima
Next Article TVLA Yazalisha Chanjo ya Kudhibiti Homa ya Kutupa Mimba kwa Mifugo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

SmartDarasa: Tunda la Miaka 40 ya COSTECH Linalobadili Elimu ya Sayansi Tanzania
Makala August 1, 2026
TVLA Yazalisha Chanjo ya Kudhibiti Homa ya Kutupa Mimba kwa Mifugo
Habari August 1, 2026
Dkt. Nchemba: TPHPA Yazidi Kuwafikia Wakulima
Habari August 1, 2026
BRELA Kutumia Maonesho Ya Nanenane Kutoa Huduma Kuhusu Mfumo Ulioboreshwa
Habari August 1, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?