Na Lucy Lyatuu
KAMPUNI ya Meli Tanzania (TASHICO) imesema usafiri wa meli ni salama na kwamba iko tayari kwa ajili ya kuuimarisha zaidi kama serikali ilivyowapa dhamana hiyo.
Aidha imesema imefanya utafiti wa kina kujua aina ya meli inayoweza kufanya kazi katika visiwa vya Pwani ikiwemo mikoa ya Tanga,Mtwara na hata visiwa jirani kama vya Comoro.
Ofisa Uhusiano wa TASHICO, Edmund Rutajama amesema hayo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa meli zote zilizopo zinafanya kazi ndani na nchi ambazo zinapakana na Tanzania.
Amesema usafiri wa meli unazidi kuimarika na kwamba meli zilizopo zinaweza pia kutumika kwa ajili ya kufanya matamasha mbalimbali hatua itakayotangaza nchi.

“Tuna meli za abiria, mizigo na hata nyingne hutumika kubeba
Makaa ya mawe na zinafanya kazi vizuri hivyo wananchi wanashauriwa kutumia usafiri huo,” amesema na kuongeza kuwa meli ya Mv Liemba hivi karibuni inatarajiwa ianze kufanya kazi.
Ofisa Masoko Mkuu wa TASHICO, Eugenia Punjila amesema Kampuninhiyo ni ya serikali ikijishughulisha kutoa huduma ya usafirishaji.
Nahodha Msaidizi wa TASHICO, Juma Chigua kampuni inajali usalama wa abiria na mizigo kuanzia mwanzo aa safari hadi mwisho.
Aidha anakaribisha watanzania kupata huduma hiyo kwa kuwa ni salama,ikiwa na uwezo aa kusafirisha.mizigo mingi kwa wakati mmoja


