Na Lucy Lyatuu, Dodoma
HOSPITALI ya Benjamini Mkapa (BMH) iliyoko mkoani Dodoma ni ya kwanza nchini kutoa huduma ya kupandikiza uume na tangu mwaka 2023 watu 14 wamepatiwa huduma hiyo hali inayosaidia kupunguza changamoto ya ndoa kuvunjika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dkt Abdallah Baja amesema hayo wakati akizungumza na waandishi na wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), waliofanya ziara katika hospitali hiyo kujionea ujenzi wa miundombinunya kisasa pamoja na huduma bobezi zitolewazo hapo.

Kuhusu kupandikiza uume amesema gharama za mtu mmoja ni sh milioni 10 ambapo wanapandikiza kwa kuweka virutubishi (e plants) ambapo mgonjwa huweza kutumia kiungo hicho kwa ufanisi zaidi.
“Virutubisho hivyo ni vya wakati wote wa uhai wa mhusika na huwezesha kufanya kazi kwa ufanisi namkwa muda kidogo kuongezeka,” amesema .
Kuhusu huduma nyingine zitolewazo hospitalini hapo, amesema zipo za kibobezi na za kibingwa ikiwa nimpamoja na upasuaji wa nyonga,ubongo na uloto.
Amesema hospitali hiyo iliyoanzishwa 2015 hadi sasa ina vitanda 40 lakini mategemeo ni kuwa na vitanda 600 na kwa siku huona zaidi ya 1200 na imekuwa hospitali bora ya kanda inayotoa huduma bora.

Amesema BMH ni hospitali ya kwanza kupandikiza uloto na ya pili kwa upandikizaji Figo kwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki,ni hospitali ya pili kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto na ya pili nchini kuweka pace marker na ya kwanza ya serikali kufanya upasuaji wa macho.
Aidha amesema ni hospitali ya kwanza kutoa huduma ya kuwafikia wananchi na kwamba ina magari matatu ambayo kwa sasa yanatoa huduma nchini Malawi na tayari Burundi imetoa huduma hiyo.


