MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waziri Sangu Awataka Waajiri Kutumia Fursa ya Msamaha wa Tozo wa NSSF
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Waziri Sangu Awataka Waajiri Kutumia Fursa ya Msamaha wa Tozo wa NSSF
Habari

Waziri Sangu Awataka Waajiri Kutumia Fursa ya Msamaha wa Tozo wa NSSF

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na MWANDISHI WETU
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amewataka waajiri nchini kutumia kikamilifu fursa ya msamaha wa tozo uliotolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kulipa madeni ya michango ya wafanyakazi, akisisitiza kuwa hatua hiyo itapunguza gharama za uendeshaji, kuongeza uzalishaji na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.
Amesema msamaha huo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira ya biashara, kuimarisha mifumo ya hifadhi ya jamii na kusikiliza changamoto za waajiri ili kuongeza tija katika sekta binafsi na sekta ya ajira kwa ujumla.
Habari Picha 12643
Waziri Sangu ametoa wito huo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa 67 wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), ambapo pia alishuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya NSSF na ATE, yenye lengo la kuimarisha ushirikiano, kubadilishana taarifa na uzoefu, pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo kwa manufaa ya waajiri, wafanyakazi na taifa.
Waziri Sangu amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake imara unaoendelea kuimarisha uchumi na kuboresha mazingira ya kazi nchini, akibainisha kuwa sekta ya ajira imeendelea kukua kutokana na sera madhubuti na ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi.
Habari Picha 12639
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amesema msamaha huo ulioanza kutekelezwa Juni mosi, 2026 hadi Desemba 31, 2026 unalenga kutoa unafuu kwa waajiri, kupunguza gharama na kuwawezesha zaidi katika uzalishaji.
Mshomba ameongeza kuwa ushirikiano kati ya NSSF na ATE utaimarisha utoaji wa elimu ya hifadhi ya jamii na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa mifumo ya kinga ya kijamii kwa waajiri na wafanyakazi.
Habari Picha 12640
Naye, Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Suzanne Ndomba-Doran, amepongeza uamuzi wa NSSF wa kutoa msamaha wa adhabu na tozo, akisema hatua hiyo ni muhimu kwa waajiri kwani inawapa nafasi ya kurekebisha na kutimiza wajibu wao wa kisheria bila kuathiri kwa kiasi kikubwa uendelevu wa biashara zao.
Amebainisha kuwa msamaha huo unaakisi ushirikiano wenye tija kati ya Serikali na taasisi za hifadhi ya jamii katika kuimarisha utii wa sheria, kuongeza usajili na michango, pamoja na kulinda maslahi ya wafanyakazi.
“Tunawahimiza waajiri kuitumia ipasavyo fursa hii kurekebisha hali zao za utii wa michango bila kuchelewa,” amesema.
Ameongeza kuwa ATE imeendelea kusambaza taarifa za msamaha huo kwa wanachama wake kupitia mifumo yake ya mawasiliano, sambamba na kuendelea kutoa elimu na hamasa kwa waajiri ili kuhakikisha wanaitumia fursa hiyo kwa manufaa ya uendelevu wa biashara na ustawi wa sekta ya ajira kwa ujumla.
Habari Picha 12641
Habari Picha 12642

You Might Also Like

Kaguo Ataja Mbinu Mpya Ukwepaji Kodi Kwenye Mafuta

TASU yaiomba serikali inunue meli kutoa ajira kwa mabaharia

Vijana Wahimizwa Kuweka Akiba

Utafiti Wa Nguvu Kazi, Mapato Ya Kaya Kutoa Taswira Mpya Ya Maendeleo

TARI Mlingano Yaleta Mapinduzi ya Mkonge, Viungo na Sayansi ya Udongo Tanzania

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article PPRA Yahimiza Makundi Maalum Kunufaika na Zabuni za Serikali
Next Article Huduma Ya Kupandikiza Uume Benjamin Mkapa Sh mil 10
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TTCL  Yatumia Tamasha La Kizimkazi Kueleza  Wananchi Fursa Wanazotoa
Makala August 15, 2026
Rais Samia Afurahishwa Na Huduma za NSSF
Habari August 13, 2026
  VETA Yashiriki Tamasha La Kizimkazi
Habari August 13, 2026
Vijana Watakiwa Kuanza Utekelezaji Wa Mipango Waliyonayo
Habari August 12, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?