MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: PPRA Yahimiza Makundi Maalum Kunufaika na Zabuni za Serikali
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > PPRA Yahimiza Makundi Maalum Kunufaika na Zabuni za Serikali
Habari

PPRA Yahimiza Makundi Maalum Kunufaika na Zabuni za Serikali

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imewahimiza vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi kujisajili katika mfumo wa ununuzi wa umma ili kunufaika na fursa za zabuni za serikali.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Dennis Simba, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyomalizika jijini Dodoma, ambapo amesema Serikali imeweka mazingira rafiki ya ushiriki wa wananchi katika shughuli za kiuchumi kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 na kanuni zake za mwaka 2024.
Simba amesema sheria hiyo, ambayo aliitaja kuwa ya kizalendo, imeelekeza taasisi zote za umma kutenga asilimia 30 ya bajeti zao za ununuzi kwa ajili ya makundi maalum ya vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.
Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika na matumizi makubwa ya fedha za umma kupitia fursa za zabuni zinazotolewa na serikali.
“Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake yaliyowezesha kupitishwa kwa sheria hii ambayo imefungua milango ya ushiriki mpana wa wananchi katika biashara na serikali.
Hii ni fursa muhimu kwa Watanzania,” amesema Simba.
Amebainisha kuwa hadi sasa zaidi ya vikundi 8,700 vimesajiliwa katika mfumo wa kitaifa wa ununuzi wa umma kielektroniki (NeST), huku thamani ya zabuni zilizotolewa kwa makundi maalum ikifikia takribani Sh bilioni 50 na mikataba iliyosainiwa ikizidi Sh bilioni 45.
Aidha, amesema PPRA kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Ofisi ya Rais imeendelea kutoa elimu nchini kote ili kuhakikisha wananchi wanaelewa na kutumia fursa hizo ipasavyo.
Amewataka pia wanahabari kuendelea kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kujisajili katika mfumo huo, akisisitiza kuwa hakuna ubaguzi katika upatikanaji wa zabuni za serikali.
Simba amehitimisha kwa kuwataka wadau wa sekta binafsi kushiriki Kongamano la Ununuzi wa Umma litakalofanyika Arusha mwishoni mwa Julai, likilenga kujadili mafanikio, changamoto na maboresho ya mfumo huo.

You Might Also Like

SEforALL Kuimarisha Ushirikiano Upatikanaji Nishati Endelevu

TASU yaiomba serikali inunue kutoa ajira kwa mabaharia

Mbogamboga Na Vitunguu Vyaingiza Sh. Milioni 370 Kwa Miaka Minne

Mkutano wa Mawaziri wa SADC Wahitimishwa Pretoria

MOI Yatoa Huduma Mpya Bobezi Tisa Kwa Mwaka 2025 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article VETA  Yapongezwa Kwa Kuibua Vipaji Kwa Vijana  
Next Article Waziri Sangu Awataka Waajiri Kutumia Fursa ya Msamaha wa Tozo wa NSSF
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TTCL  Yatumia Tamasha La Kizimkazi Kueleza  Wananchi Fursa Wanazotoa
Makala August 15, 2026
Rais Samia Afurahishwa Na Huduma za NSSF
Habari August 13, 2026
  VETA Yashiriki Tamasha La Kizimkazi
Habari August 13, 2026
Vijana Watakiwa Kuanza Utekelezaji Wa Mipango Waliyonayo
Habari August 12, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?