MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Qwaray Aipongeza VETA kwa Kukuza Ujuzi wa Vijana
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Qwaray Aipongeza VETA kwa Kukuza Ujuzi wa Vijana
Habari

Qwaray Aipongeza VETA kwa Kukuza Ujuzi wa Vijana

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray, ameipongeza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa mchango wake katika kuwajengea vijana ujuzi unaowawezesha kujiajiri na kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi.
Akizungumza baada ya kutembelea banda la VETA katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma Juni 22, 2026, Qwaray amesema Serikali imejikita katika kuwawezesha vijana kujiajiri, jambo ambalo litafanikiwa zaidi kupitia uwekezaji mkubwa katika elimu ya ufundi na stadi za kazi.
“Vijana wanapopata ujuzi wa ufundi wanakuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi badala ya kusubiri ajira za Serikali. Hivyo, ni muhimu kuendelea kuwekeza katika vyuo vya VETA ili kuongeza fursa za ajira na uzalishaji,” amesema.
Habari Picha 12575
Qwaray pia ameipongeza VETA kwa kutoa mafunzo kwa watu wenye mahitaji maalum na kwa juhudi zake za kuzalisha bidhaa mbalimbali kupitia kampuni tanzu ya VETA Ujuzi, hatua inayochangia kukuza uchumi na kuongeza thamani ya mafunzo yanayotolewa.
Amesema wahitimu wa elimu mbalimbali, ikiwemo kidato cha nne na elimu ya juu, wanapaswa kutumia fursa zinazotolewa na VETA kupata stadi zinazowawezesha kujiajiri na kuanzisha shughuli za uzalishaji.
Aidha, amebainisha kuwa maendeleo ya ujuzi kwa wananchi ni nguzo muhimu katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga uchumi wa kisasa unaotegemea maarifa na ubunifu.
Habari Picha 12578
VETA ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza Juni 16, 2026, kufunguliwa rasmi Juni 17 na Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, na yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 23, 2026.

You Might Also Like

Zungu Achaguliwa Kuwa Spika Mpya Wa Bunge La 13

Bodi ya mkonge kutoa ajira kwa watu 10,000 ifukapo 2030

Baraza la uuguzi na ukunga lawakaribisha wenye malalamiko

DC Atoa Wito kwa Tume ya Kurekebisha Sheria Kuzingatia Sheria Ndogondogo za Halmashauri

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Hiari Upo Kwa Ajili ya Watanzania – Kabonaki

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mkomi Atembelea Banda la PSSSF
Next Article Katibu Mkuu Uchukuzi Aipongeza TASAC,  Kuelimisha Wananchi 
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mfumo Wa Kidijitali Wa PSSSF Wamvutia Mkurugenzi Wa BOT
Habari August 5, 2026
FAO Yasisitiza Kutowapa Mifugo Dawa Bila Maelekezo Ya Watalaam
Habari August 5, 2026
Balozi Wa Kudumu Wa Mashirika Ya UN Atembelea FAO Nanenane
Habari August 5, 2026
Wadau Wamiminika Banda La REA Katika Maonesho Ya Nanenane  2026
Habari August 5, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?