MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ridhiwani Aipongeza EWURA kwa Utoaji wa Huduma kwa Wananchi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ridhiwani Aipongeza EWURA kwa Utoaji wa Huduma kwa Wananchi
Habari

Ridhiwani Aipongeza EWURA kwa Utoaji wa Huduma kwa Wananchi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa juhudi zake katika kusimamia sekta za nishati na maji pamoja na kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
Ridhiwani ametoa pongezi hizo leo Juni 17, 2026, alipotembelea banda la EWURA katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya kupata maelezo kuhusu shughuli zinazotekelezwa na mamlaka hiyo, Ridhiwani amesema ameridhishwa na namna EWURA inavyotekeleza majukumu yake na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Habari Picha 12407
“Hongereni sana kwa kazi kubwa mnayoifanya,” amesema Waziri huyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa EWURA, Hawa Mniga, amesema mamlaka hiyo imejitokeza katika maadhimisho hayo ili kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma zake pamoja na kupokea na kushughulikia kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika sekta za nishati na maji.
Ameeleza kuwa wananchi wanaotembelea banda la EWURA wanapata fursa ya kufahamu majukumu ya mamlaka hiyo, kuuliza maswali na kuwasilisha changamoto zao kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa haraka.
“Tupo hapa kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi na kushughulikia kero pamoja na migogoro inayohusiana na masuala ya nishati,” amesema Mniga.
Habari Picha 12408
Aidha, amesema ushiriki wa EWURA katika Wiki ya Utumishi wa Umma unalenga kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki na wajibu wao katika sekta zinazodhibitiwa na mamlaka hiyo, sambamba na kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa kwa jamii.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu yameanza Juni 16 na yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 25, 2026.

You Might Also Like

NIC Yatoa Elimu ya Bima Kwenye Kijiji cha Bima, Maonesho ya Madini Geita

Lukuvi Asema 2024 Bangi Ilivunja Rekodi, Tani Zaidi Ya 2000 Zilikamatwa

Makalla Aeleza Jinsi CCM Ilivyosimamisha Nchi Mchakato Kura Za Maoni

Mabalozi Wa Utalii Waahidi Kuulinda Ushoroba Wa Kwakuchinja

Wagombea Wa CCM Dodoma Mjini Waanza Kujinadi kwa Wajumbe

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article VETA Yazalisha Bidhaa 825, Zinauzwa Ndani Na Nje Ya Nchi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

VETA Yazalisha Bidhaa 825, Zinauzwa Ndani Na Nje Ya Nchi
Habari June 17, 2026
 Mfumo Wa REA  Wa Digital Platform  Wapongezwa Na Waziri Kikwete
Habari June 17, 2026
Ridhiwani Kikwete Atembelea Banda la REA, Aipongeza Kasi ya Usambazaji Umeme Vijijini
Habari June 17, 2026
Ridhiwani Aipongeza TEA kwa Kuimarisha Elimu Nchini
Habari June 17, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?