MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ridhiwani Aipongeza TEA kwa Kuimarisha Elimu Nchini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ridhiwani Aipongeza TEA kwa Kuimarisha Elimu Nchini
Habari

Ridhiwani Aipongeza TEA kwa Kuimarisha Elimu Nchini

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DODOMA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, ameipongeza Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa mchango wake katika kuimarisha sekta ya elimu nchini kupitia usimamizi wa Mfuko wa Elimu wa Taifa na utoaji wa elimu kwa umma kuhusu shughuli zake.

Pongezi hizo alizitoa jana alipotembelea banda la TEA katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Akiwa katika banda hilo, Kikwete amesema anatambua kazi kubwa inayofanywa na TEA katika kuisaidia Serikali kuboresha elimu kwa kutafuta vyanzo vya rasilimali fedha na vifaa vinavyosaidia kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

“Nazifahamu kazi zinazofanywa na TEA. Endeleeni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yenu ili watu wengi zaidi waweze kufahamu mchango wa mamlaka hii katika maendeleo ya elimu nchini,” amesema Kikwete.

Awali, Ofisa Uhusiano wa TEA, Eliafile Solla, amesema mamlaka hiyo inasimamia Mfuko wa Elimu wa Taifa wenye jukumu la kutafuta na kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali fedha na vifaa kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya elimu nchini.

Amefafanua kuwa rasilimali hizo husambazwa katika shule na taasisi mbalimbali za elimu kwa lengo la kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia, hivyo kuongeza ubora na upatikanaji wa elimu kwa usawa.

“TEA ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Tumeshiriki maonesho haya ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yetu na miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa,” amesema Solla.

Ameongeza kuwa watumishi wa TEA wamejipanga kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, hususan katika kutafuta rasilimali zitakazosaidia juhudi za Serikali za kuboresha sekta ya elimu nchini.

You Might Also Like

Serikali Kusaini Muongozo Wa Kima Cha Chini Cha Mshahara Kwa Sekta Binafsi

Udiwani Kata Ya Mbabala Kizungumkuti

Taifa Gas Yaendelea Kuongoza Kampeni ya Nishati Safi kwa Taasisi na Sekta ya Utalii Tanzania

Rais Dkt Mwinyi Afika Katika Dua ya Kumuombea Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Pili

Mtasingwa Aitaka Serikali Kuwatengea Eneo Wafanyabiashara wa Senene Bukoba

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mhitimu Mwenye Ulemavu Aivutia Serikali kwa Ubunifu wa Ramani VETA
Next Article Ridhiwani Kikwete Atembelea Banda la REA, Aipongeza Kasi ya Usambazaji Umeme Vijijini
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ridhiwani Aipongeza EWURA kwa Utoaji wa Huduma kwa Wananchi
Habari June 17, 2026
VETA Yazalisha Bidhaa 825, Zinauzwa Ndani Na Nje Ya Nchi
Habari June 17, 2026
 Mfumo Wa REA  Wa Digital Platform  Wapongezwa Na Waziri Kikwete
Habari June 17, 2026
Ridhiwani Kikwete Atembelea Banda la REA, Aipongeza Kasi ya Usambazaji Umeme Vijijini
Habari June 17, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?