MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: NHC Kuendelea Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Kimkakati Ya Ujenzi Wa Nyumba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > NHC Kuendelea Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Kimkakati Ya Ujenzi Wa Nyumba
Habari

NHC Kuendelea Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Kimkakati Ya Ujenzi Wa Nyumba

Author
By Author
Share
4 Min Read

Na Lucy Lyatuu,Dodoma

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), ambapo miradi kadhaa ya kimkakati ikitarajiwa kukamilika ndani ya mwaka 2026 na mingine kuanza rasmi mwaka wa fedha 2026/27.

Akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka 2026/27, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo amesema S NHC imeendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya nyumba, biashara na uwekezaji inayolenga kuongeza upatikanaji wa makazi bora pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa miji mbalimbali nchini.

Dkt. Akwilapo amesema ujenzi wa nyumba 422 katika mradi wa Kawe 711 jijini Dar es Salaam wenye thamani ya sh bilioni 169 umefikia asilimia 85 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 30, 2026.

Aidha amesema, mradi wa nyumba 196 wa Golden Premier Residence (GPR) wenye thamani ya sh bilioni 127 umefikia asilimia 50 huku ukitarajiwa kukamilika mwaka 2027.

Waziri amesema Serikali pia inaendelea na maandalizi ya utekelezaji wa miradi mipya ya makazi kupitia mpango wa nyumba 5,000 wa Samia Housing Scheme katika maeneo ya Mtoni Kijichi na Kawe jijini Dar es Salaam pamoja na Medeli na Iyumbu jijini Dodoma.

“Katika mwaka 2026/27, Shirika litaendelea na ujenzi wa nyumba katika miradi ya Samia Housing Scheme sambamba na kuanza utekelezaji wa miradi mipya katika maeneo ya Njedengwa Dodoma, Urafiki Dar es Salaam, Makongoro Mwanza na Sokoine Complex Arusha,” amesema Dkt. Akwilapo.

Kwa upande wa nyumba za gharama nafuu, Waziri Akwilapo amesema NHC imekamilisha maandalizi ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 800 katika maeneo ya Salama Creek Kigamboni, Sabasaba Morogoro, Iyumbu Dodoma na Buswelu Mwanza, ambapo utekelezaji rasmi utaanza mwaka 2026/27.

Mbali na sekta ya makazi, Waziri huyo amesema NHC inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya majengo ya biashara nchini, hatua inayochochea shughuli za kiuchumi pamoja na kuongeza thamani ya maeneo ya mijini.

Ameitaja Miradi hiyo ni pamoja na Meru View Shops Arusha iliyofikia asilimia 52, Tabora Commercial Complex asilimia 46, Singida 2F Plaza asilimia 85, Mkwakwani Commercial Complex Tanga asilimia 40, Kashozi Commercial Complex Kagera asilimia 65, Uluguru Plaza Morogoro asilimia 42 na Iringa Commercial Complex asilimia 40.

Aidha, Serikali imeeleza kuwa miradi ya biashara na ofisi katika maeneo ya Masasi, Mtanda Lindi na Zongomela Kahama imekamilika huku maandalizi ya mwisho ya miradi ya Usa River na Ngarenaro yakiendelea.

Katika eneo la ubia, Mhe. Dkt. Akwilapo amesema NHC linaendelea kusimamia miradi 21 ya ubia yenye thamani ya shilingi bilioni 351 ambapo miradi mitatu imekamilika na mingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji kwa wastani wa asilimia 56.

Amesema pia Shirika linaendelea kutwaa na kufufua miradi iliyokuwa imesimama kwa muda mrefu ili kuhakikisha uwekezaji huo unaleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Kati ya miradi 24 iliyokuwa imesimama, miradi 13 imekamilika huku mingine ikiendelea kushughulikiwa.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amesema NHC limeendelea kuimarisha utendaji wake wa kifedha ambapo hadi Mei 15, 2026 limefanikiwa kupunguza madeni kutoka sh bilioni 27.98 mwaka 2024/25 hadi sh bilioni 19 mwaka 2025/26.

Pia, Shirika limeendelea na mpango wa ukarabati wa nyumba zake ambapo nyumba 1,283 kati ya nyumba 1,600 zilizopangwa kukarabatiwa tayari zimekamilika sawa na asilimia 80 ya lengo.

Kuhusu wa miradi ya ukandarasi na ushauri elekezi, amesema NHC limekamilisha ujenzi wa majengo nane ya Ofisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma pamoja na jengo la Soko la Madini la Tanzanite Mirerani Manyara.

Kadhalika, ujenzi wa majengo ya TCRA Dodoma umefikia asilimia 73 huku mradi wa Zanzibar ukiwa umefikia asilimia 50.

You Might Also Like

THBUB Mdau Mkubwa Utekelezaji Wa Majukumu 

Dkt. William Ruto Aipongeza NSSF Tanzania Kwa Uwekezaji wa Dola zaidi ya Milioni 51 Nairobi

TMDA Kudhibiti Bidhaa Za Tumbaku Ili Wananchi Wasiendelee Kupata Madhara

Dkt. Ndumbaro : Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Imefanikiwa 

Chalamila: Serikali Imewekeza Kupatikana Wataalamu Wa Usingizi, Yapunguza Vifo Vinavyotokana Na Upasuaji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kutokulipa Kodi Ya Pango La Ardhi Unakosa Sifa Za Kugombea Nafasi Za Uongozi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Kutokulipa Kodi Ya Pango La Ardhi Unakosa Sifa Za Kugombea Nafasi Za Uongozi
Habari May 28, 2026
Tanzania Hakuna Tatizo La Kidini Wala Kiimani-JMAT
Habari May 26, 2026
TUCTA Yawataka Wanahabari Kueneza Elimu ya Fidia kwa Wafanyakazi
Habari May 26, 2026
JOWUTA Yataka Wanahabari Wasajiliwe WCF
Habari May 26, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?