MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wizara Ya Elimu Yaomba Kuidhinishiwa Trilioni 2.3
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wizara Ya Elimu Yaomba Kuidhinishiwa Trilioni 2.3
Habari

Wizara Ya Elimu Yaomba Kuidhinishiwa Trilioni 2.3

Author
By Author
Share
4 Min Read

Na Lucy Lyatuu,Dodoma

WIZARA  ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeiomba  Bunge  kuidhinisha jumla ya takribani Sh trilioni 2.3 kwa ajili ya kuimarisha sekta ya elimu nchini, ikilenga kuboresha miundombinu, kuongeza ubora wa ufundishaji na kuendeleza matumizi ya teknolojia katika elimu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema hayo wakati akiwasilisha Bungeni  makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara na kwamba    fedha hizo zitaelekezwa katika miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa madarasa, mabweni, maabara, vyuo vya ufundi pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kuipa kipaumbele sekta ya elimu kutokana na mchango wake mkubwa katika kujenga rasilimali watu wenye ujuzi na uwezo wa kuchangia katika uchumi wa taifa.

Aidha, amebainisha kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo itaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ili kuhakikisha wanafunzi wote nchini wanapata mazingira bora ya kujifunzia bila changamoto za msingi.

Ameeleza kuwa Serikali imepanga kuongeza ufadhili wa miradi ya utafiti na ubunifu kutoka miradi 80 hadi 109, kwa kuzingatia maeneo ya kipaumbele ya kitaifa. Miradi hiyo inalenga kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, uchumi wa bluu, uvuvi, maji, kilimo, afya na maendeleo ya viwanda.

Katika hatua nyingine, Serikali kupitia taasisi za elimu ya juu na elimu ya ufundi itatekeleza jumla ya miradi 1,390 ya utafiti katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, biashara, kilimo, uongozi, ushirika, teknolojia, uvuvi, ardhi, mazingira na usanifu majengo. Hatua hii inalenga kuimarisha msingi wa maarifa na ubunifu unaohitajika katika kukuza uchumi wa taifa.
Aidha, Serikali imepanga kuchapisha jumla ya tafiti 2,497 katika majarida ya kitaifa na kimataifa ili kuongeza usambazaji wa maarifa, kuchochea mijadala ya kitaaluma na kuhakikisha matokeo ya utafiti  yanatumika katika kutatua changamoto.
Aidha, Serikali imepanga kuchapisha jumla ya tafiti 2,497 katika majarida ya kitaifa na kimataifa ili kuongeza usambazaji wa maarifa, kuchochea mijadala ya kitaaluma na kuhakikisha matokeo ya utafiti yanatumika katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi.
Katika kuimarisha miundombinu ya utafiti, Serikali itajenga uwezo wa maabara katika taasisi tano za utafiti na maendeleo ili ziwe maabara za rufaa kwa utafiti wa viwanda na ubunifu wa kisasa. Pia, itaimarisha ushirikiano kati ya taasisi za utafiti, elimu ya juu na sekta ya viwanda ili kuongeza mchango wa sayansi katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Serikali pia itaendelea kuhamasisha wabunifu na kuongeza idadi ya wanufaika wanaopata mikopo kupitia Mfuko wa Ubia na Ubiasharishaji wa Ubunifu wa Samia (Samia Innovation Commercialization Fund). Kupitia mpango huo, vyuo vitano vya Maendeleo ya Wananchi vitapatiwa vituo vya ubunifu ili kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana.
Katika kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia, Serikali itaimarisha utafiti na udhibiti wa matumizi ya teknolojia ya nyuklia katika sekta mbalimbali. Aidha, itaendelea kukagua vituo 900 vyenye vyanzo vya mionzi na kupima viwango vya mionzi kwa wafanyakazi 2,110 wanaofanya katika mazingira havo ili kulinda afva .

You Might Also Like

Profesa Nombo: Ushirikiano wa VETA, Sekta Binafsi Waimarisha Mafunzo ya Ufundi Stadi

Profesa Ndunguru: Teknolojia ya Vinasaba Yafungua Ukurasa Mpya Katika Kilimo

VETA Mtwara Watua Na Mwani Maadhimishilo Ya Miaka 30

Waziri Sangu Aagiza Hatua Kali kwa Waajiri Wanaokwepa Kuwasilisha Michango NSSF

Ulega Ataka Ushirikiano Miradi Ya Kimkakati Ikamilike Kwa Wakati

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Dkt. William Ruto Aipongeza NSSF Tanzania Kwa Uwekezaji wa Dola zaidi ya Milioni 51 Nairobi
Next Article Kesi 100 Za Wananchi Zasikilizwa Na Kupatiwa Suluhu Katiba Na Sheria
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

IITA Yawekeza Bilioni 410 Tanzania Kuimarisha Kilimo, Utafiti
Habari May 9, 2026
Vyuo Vikuu Vyahitaji Mkakati Madhubuti wa Tafiti — Yanda
Habari May 8, 2026
Asilimia 26 Ya Wanawake Ndio Wanaoamini Kuwa Na Uhuru Wa Kufanya Maamuzi Ya Kufanya Shughuli Za Uchumi
Habari May 8, 2026
Kesi 100 Za Wananchi Zasikilizwa Na Kupatiwa Suluhu Katiba Na Sheria
Habari May 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?