Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Kenya, William Ruto ameusifu uwekezaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa Tanzania unaoendelea jijini Nairobi, akieleza kuwa ni mfano bora wa matumizi sahihi ya akiba za wanachama katika kukuza uchumi na maendeleo ya kikanda.
Akihutubia Bunge leo Jumanne Mei 5, 2026 jijini Dodoma, Ruto amesema uwekezaji huo unaonesha namna taasisi za ndani zinavyoweza kuwa chachu ya maendeleo siyo tu katika nchi zao bali pia ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema hatua ya NSSF kuwekeza nchini Kenya inaimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili, huku ikitoa fursa za ajira na kukuza sekta mbalimbali za uzalishaji.
Ruto amesisitiza kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii barani Afrika inapaswa kuendelea kuelekeza rasilimali zake katika miradi yenye tija, ili kuongeza thamani ya akiba za wanachama na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kikanda.


