MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waziri Aweso Aainisha Mikakati ya Kuboresha Huduma ya Maji
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Waziri Aweso Aainisha Mikakati ya Kuboresha Huduma ya Maji
Uncategorized

Waziri Aweso Aainisha Mikakati ya Kuboresha Huduma ya Maji

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, ametangaza mikakati kabambe ya kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama nchini wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni, jijini Dodoma.
Amesema Serikali itaendelea kuimarisha huduma ya maji kwa kutumia teknolojia za kisasa, kupanua vyanzo vya fedha na kushirikisha sekta binafsi.
Habari Picha 11978
Ili kuongeza kasi ya miradi, Wizara imeanza maandalizi ya Hati Fungani ya Sekta ya Maji itakayovutia uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Aweso amebainisha kuwa Dira 2050 inalenga asilimia 70 ya uwekezaji kutoka sekta binafsi, huku Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002 (Toleo la 2025) ikifungua nafasi kwa wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu.
Aidha, Mfuko wa Taifa wa Maji utaimarishwa ili kuongeza fedha za miradi na maendeleo ya vyanzo vya maji.
Katika kuboresha huduma, Wizara itaongeza matumizi ya TEHAMA ikiwemo mita za kidijitali (Mita Janja) na maombi ya huduma mtandaoni.
Hadi Aprili 2026, jumla ya mita 23,156 zimefungwa, kutoka 13,526 mwaka 2025, huku lengo likiwa kufunga mita 1,114,133 mijini ifikapo 2030.
Teknolojia hii inalenga kuondoa changamoto za ankara zisizo sahihi na upotevu wa maji.
Aidha, Waziri amesisitiza ushirikiano wa sekta mbalimbali katika matumizi ya rasilimali za maji, ikiwemo ujenzi wa mabwawa ya matumizi ya pamoja na uvunaji wa maji ya mvua.
Kwa mwaka 2026/2027, Wizara imeomba kuidhinishiwa Sh. Trilioni 1.12, ambapo Sh. Bilioni 80.65 ni matumizi ya kawaida na Trilioni 1.03 ni kwa maendeleo.
Mikakati hiyo inalenga kuhakikisha huduma bora na endelevu ya maji kwa wananchi wote.

You Might Also Like

Wasira akipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  kwa kuenzi Falsafa za Baba wa Taifa

Trilioni 1.2 kuboresha miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam

Wananchi Wachagua Viongozi Serikali Za Mitaa

Bil.19 kusambaza umeme vitongojini Tabora

Profesa Kabudi Amimina Pongezi TEA

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wizara ya Maji Yawasilisha Vipaumbele 2026/2027 kwa Bajeti ya Trilioni 1.2
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wizara ya Maji Yawasilisha Vipaumbele 2026/2027 kwa Bajeti ya Trilioni 1.2
Habari May 5, 2026
CCM  Yapokea Mapendekezo Ya Tume Ya Kuchunguza Vurugu Za Uchaguzi Oktoba 25,2025
Habari May 5, 2026
Mitandao Ya Kijamii Ilinde Maadili Ya Kitanzania-Makonda
Habari May 4, 2026
Rais Samia Amkabidhi Tuzo Profesa Ndunguru kwa Kuinua Mapato, Maboresho TPHPA
Habari May 3, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?