MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: JOWUTA Yataka Vyombo vya Habari Vishirikishwe Zaidi Mei Mosi Njombe
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > JOWUTA Yataka Vyombo vya Habari Vishirikishwe Zaidi Mei Mosi Njombe
Habari

JOWUTA Yataka Vyombo vya Habari Vishirikishwe Zaidi Mei Mosi Njombe

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
NJOMBE: CHAMA cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimetaka kuongezwa kwa ushirikishwaji wa vyombo vya habari katika maandalizi na maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu 2026 yatakayofanyika mkoani Njombe.
JOWUTA, ambayo mwaka huu inashiriki kwa mara ya kwanza kama mwanachama wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), imesema pia inatarajia kutoa tuzo kwa wafanyakazi bora katika sekta ya habari.
Habari Picha 11772
Akizungumza katika kikao cha maandalizi ya Mei Mosi, mkoani Njombe, Mwenyekiti wa JOWUTA Taifa, Mussa Juma, ameipongeza Kamati ya Habari na Matangazo ya Mei Mosi kitaifa, lakini akabainisha kuwa bado ushiriki wa vyombo vya habari haujaridhisha.
Amesisitiza umuhimu wa kuvishirikisha zaidi vyombo mbalimbali ikiwemo magazeti, redio, televisheni na mitandao ya kijamii katika utoaji wa taarifa na matangazo.
Ameongeza kuwa maudhui ya matangazo yanapaswa kuangazia vivutio na fursa zilizopo mkoani Njombe ili kuutangaza zaidi mkoa huo.
Juma amesema JOWUTA, yenye wanachama zaidi ya 400 nchi nzima, iko tayari kushirikiana na kamati za Mei Mosi kuimarisha utoaji wa taarifa na kuhamasisha ushiriki wa wananchi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa RAAWU, Jane Mihanji, amehimiza umuhimu wa kugharamia magazeti yanayochapisha matoleo maalum ya Mei Mosi, akieleza kuwa yamekuwa yakitoa makala muhimu kuhusu utekelezaji wa miradi ya serikali na sekta binafsi.
Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya, amesema maadhimisho hayo ni fursa ya kuitangaza Njombe, akitaja sekta za kilimo cha parachichi, viazi, mbao pamoja na vivutio vya utalii.
Wakati huohuo, Kamati ya maandalizi ya Mei Mosi kitaifa imetembelea ujenzi wa uwanja wa maadhimisho na kuagiza kasi iongezwe ili ukamilike ifikapo Aprili 25 mwaka huu, 2026.

You Might Also Like

Kafulila: Ushirikiano wa Sekta Binafsi na Umma Kuboresha Huduma

Viongozi Watakiwa Kuweka Haki Mbele Katika Kusimamia Masuala ya Wafanyakazi — COWTU (T)

Serikali Yasisitiza Utoaji Huduma Bora Utekelezaji Bima Ya Afya

TARI yapongezwa kwa kuwa na teknolojia bora za kilimo

Mbegu Bora za Miwa Zenye Tija ya Tani 200 kwa Hekta Zaendelea Kuwanufaisha Wakulima

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wizara Yapanga Kunufaika Na Maarifa Ya Mabalozi Wastaafu
Next Article WASICHANA WAANDIKA HISTORIA MPYA KWENYE MASOMO YA SAYANSI MKOANI SONGWE
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Habari July 30, 2026
Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Habari July 30, 2026
Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa Msongo Wa Kilovolti 400 Chalinze -Dodoma Mbioni Kukamilika
Habari July 29, 2026
Kutoka Wazo Rahisi Hadi Mapinduzi ya Kilimo: Safari ya Rafiki Planter Inayosimulia Miaka 40 ya COSTECH
Makala July 28, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?