MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tume Ya Madini Kufuta  Leseni 40 Za Utafutaji Madini 
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tume Ya Madini Kufuta  Leseni 40 Za Utafutaji Madini 
Habari

Tume Ya Madini Kufuta  Leseni 40 Za Utafutaji Madini 

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Lyatuu, Dodoma

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde ameielekeza Tume ya Madini kufuta jumla ya leseni 40 za utafiti wa madini ambao wameshindwa kuendeleza leseni hizo  huku akiagiza maofisa madini kusimamia sheria ya madini ipasavyo.

AIdha amesema lipo wimbi kubwa la watu kuingia kwenye leseni za wengine  hivyo ufutaji wa leseni hizo kuimarisha usimamizi wa rasilimali za madini na kuondoa wamiliki wasiotekeleza masharti ya leseni, huku akionya kuwa Serikali haitavumilia uzembe unaokwamisha maendeleo ya Sekta ya Madini pamoja na uchumi kwa ujumla.

Waziri Mavunde ameoa taarifa hiyo  jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari, akieleza kuwa leseni hizo zimefutwa baada ya wamiliki wake kushindwa kuziendeleza licha ya kupewa hati za makosa na muda wa kurekebisha kasoro zilizobainika na kwamba zitarudishwa Serikalini kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kugawa kwa wachimbaji wadogo,wawekezaji walio na utayari na makundi ya Wanawake na Vijana kupitia Programu ya Mining for A Brighter Tomorrow-MBT.

Habari Picha 11759

Amesema kuwa, tathmini ya kina iliyofanywa na Wizara ya Madini imeonesha uwepo wa ukiukwaji mkubwa wa masharti ya leseni, ikiwemo baadhi ya wamiliki kuhodhi maeneo bila kuyaendeleza, kushindwa kulipa ada stahiki, kutotekeleza wajibu wa ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content), pamoja na kushindwa kutekeleza miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR).

Kadhalika amesema mwenye leseni ana jukumu la kulinda leseni yake  na kwamba atakayeingia kwenye eneo lake aondolewe mara moja kwa mujibu wa sheria

Amesema  vitendo vya kuhodhi leseni vimekuwa chanzo kikubwa cha migogoro na kuchochea uchimbaji holela, hali inayohatarisha usalama wa wananchi, mazingira na mapato ya Serikali.

Wakati huo huo  serikali kupitia Tume ya Madini imetoa hati za makosa kwa leseni nyingine 43, zikiwemo leseni 40 za utafutaji na tatu za uchimbaji wa kati, huku wamiliki wake wakitakiwa kurekebisha kasoro ndani ya siku 30.

Amesisitiza kuwa endapo masharti hayo hayatatekelezwa ndani ya muda uliowekwa, leseni hizo zitafutwa na maeneo husika kutolewa kwa wawekezaji wengine wenye uwezo wa kuyaendeleza.

Habari Picha 11760

Mavunde amesema hatua ya kufuta leseni 40 inaashiria msimamo thabiti wa Serikali wa kuendeleza Sekta ya Madini dhidi ya uzembe na vitendo visivyo halali, huku ikifungua ukurasa mpya wa uwajibikaji na ushindani wa haki katika matumizi ya rasilimali za taifa.

You Might Also Like

TPHPA Yaleta Mapinduzi Mapya Katika Kilimo Kupitia Teknolojia ya Vinasaba

PSSSF Itaendelea Kuwekeza Kwenye Maeneo Salama Yenye Tija

Matumizi Mabaya Ya Dawa Husababisha Usugu Wa Vimelea Kwa Wanyama – Dkt. Kitimu

Watakiwa kufanya utafiti kubaini chanzo cha makosa ya walimu

Kamati Ya Bunge Yapongeza Usimikaji Mfumo Wa Kidijitali CMA

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Kushughulikia Utitiri Wa Vyama Ndani Ya Sekta Binafsi
Next Article Wizara Yapanga Kunufaika Na Maarifa Ya Mabalozi Wastaafu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Yatoa Mwelekeo Maandalizi AFCON 2027, Yaimarisha Miundombinu Nchini
Habari April 17, 2026
Makampuni 100 kushiriki maonesho ya OSHA Njombe
Habari April 17, 2026
Ufaulu  Wa   Somo La Hisabati  Shida Ya Taifa- Wanu
Habari April 16, 2026
Ofisi ya Rais Mipango Yaomba Bilioni 144.85 kwa Bajeti 2026/27
Habari April 16, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?