MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kanzidata ya Taifa ya Uwekezaji Yalenga Kuboresha Takwimu na Kuvutia Wawekezaji
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kanzidata ya Taifa ya Uwekezaji Yalenga Kuboresha Takwimu na Kuvutia Wawekezaji
Habari

Kanzidata ya Taifa ya Uwekezaji Yalenga Kuboresha Takwimu na Kuvutia Wawekezaji

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Viti Maalum, Dkt. Neema Majule, amehoji Serikali kuhusu mpango wa kusajili wawekezaji wote nchini kupitia Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi (TISEZA), hatua inayolenga kuwa na kanzidata sahihi ya uwekezaji.
Akizungumza bungeni, Dkt. Majule ameitaka Serikali kufafanua mikakati yake kuhakikisha wawekezaji wote, wa ndani na wa nje, wanajiandikisha rasmi.
Lengo ni kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi zitakazosaidia kupanga na kusimamia uchumi wa Taifa.
Akijibu, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, amesema TISEZA inaendelea kusajili miradi ya uwekezaji kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, ikiwemo kiwango cha mtaji.
Amesema hadi sasa, Serikali kupitia TISEZA imesajili miradi 14,209 na kutoa vyeti vya utambuzi.
“Mheshimiwa Spika, katika kuendana na maendeleo ya teknolojia ya kidigitali, TISEZA imekamilisha ujenzi wa Mfumo wa Kanzidata ya Taifa ya Uwekezaji wa Sekta Binafsi, utakaounganisha mifumo ya taasisi mbalimbali zinazohusika na usajili wa makampuni ya wawekezaji,” amesema Dkt. Chaya.
Ameongeza kuwa mfumo huo utaboresha upatikanaji wa takwimu sahihi, hususan kuhusu mitaji iliyowekezwa na ajira zinazozalishwa na sekta binafsi.
Serikali pia inaendelea na kampeni ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani kupitia wazawa, sambamba na kuwahamasisha wawekezaji wasiosajiliwa kujiandikisha rasmi.
Kuhusu vigezo vya usajili, Dkt. Chaya amesema wawekezaji wazawa wanapaswa kuwa na mtaji wa angalau dola 50,000 (takriban Sh. milioni 125), huku wawekezaji wa kimkakati wa ndani wakitakiwa kuwa na dola milioni 50.
Kwa wawekezaji wa nje, mtaji wa chini ni dola 500,000 kwa wale wa kawaida na dola milioni 500 kwa wawekezaji wa kimkakati.
Aidha, Naibu Waziri amebainisha kuwa Serikali imeweka vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi ili kuwavutia wawekezaji zaidi kuwekeza na kujisajili rasmi kupitia TISEZA.
Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza uwazi, ufuatiliaji na mchango wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa Taifa.

You Might Also Like

Tanzania, Afrika Kusini Zakubaliana Kuharakisha Makubaliano ya Ushirikiano

Utiaji Saini Mkataba Wa Ujenzi Jengo La TUGHE Wafanyika

Tutumie Mitandao Kwa Matumizi Yenye Manufaa – Kilimbe

Asilimia 86.2 ya Wanawake  wanajishughulisha na shughuli za madini

Waziri wa Vijana akutana na Mwita wa Zanzibar

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wananchi wa Kasulu Vijijini Wananufaika na Uwekezaji Makere Forest Reserve
Next Article Serikali Yaimarisha Vitengo vya Tathmini na Ufuatiliaji Kuwa Huduma Bora kwa Wananchi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ubunifu Wa Majengo Watakiwa Kuzingatia Tija Na Gharama Nafuu
Habari April 11, 2026
Waziri Ulega aridhishwa na miradi ya dharura TANROADS
Habari April 11, 2026
Mbunge Majule ataka wanawake wapewe elimu ya fedha na mitaji
Habari April 11, 2026
Mbunge Msita Ataka Ukarabati Wa Haraka Barabara Zilizoharibiwa Na Mvua
Habari April 11, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?