MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TASFAM Yawawezesha Wanawake wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kuadhimisha Siku ya Mwanamke
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TASFAM Yawawezesha Wanawake wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kuadhimisha Siku ya Mwanamke
Habari

TASFAM Yawawezesha Wanawake wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kuadhimisha Siku ya Mwanamke

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WANAWAKE wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wameungana na wanawake wengine kuadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani katika maadhimisho yaliyofanyika wilayani Kongwa, mkoani Dodoma.
Akizungumza baada ya maadhimisho hayo, Kaimu Mwenyekiti wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), Joyce Mamkwe, amesema maadhimisho ya mwaka huu 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Haki na usawa kwa wanawake na wasichana, msingi jumuishi wa kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.’
Habari Picha 11373
Amesema kaulimbiu hiyo inalenga kuhimiza ushiriki wa wanawake katika mnyororo mzima wa thamani katika sekta mbalimbali za maendeleo ili kuchochea ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
Mamkwe ameeleza kuwa wanawake wa wizara hiyo wameshiriki maadhimisho hayo kwa ufadhili wa Mradi wa Kuendeleza Usimamizi wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Bahari Tanzania (TASFAM).
“Leo Wizara ya Mifugo na Uvuvi tupo Kongwa kuadhimisha siku hii muhimu katika maisha ya mwanamke kuanzia anapozaliwa hadi anapokuwa mtu mzima.
“Tunashukuru mradi wa TASFAM ambao umetuwezesha kufika hapa na kujumuika na wanawake wenzetu,” amesema.
Ameongeza kuwa mradi huo una programu ya kuendeleza shughuli za uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji katika ukanda wa Pwani, huku wanawake wakitarajiwa kuwa sehemu muhimu ya wanufaika na washiriki wa shughuli hizo.
Habari Picha 11374
Kwa upande wake, Teddy Salema kutoka Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, ameushukuru mradi huo kwa kuwawezesha kushiriki maadhimisho hayo.
Amesema jamii inapaswa kutambua uwezo wa wanawake kwani wakipewa nafasi na kuwezeshwa wanaweza kuchangia maendeleo makubwa ya taifa.
“Wanawake wakipewa nafasi wanafanya mambo makubwa. Hata Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha uwezo mkubwa wa uongozi,” amesema.
Salema ameongeza kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika sekta ya mifugo, hususan katika ufugaji, chanjo pamoja na uzalishaji wa malisho na vyakula vya mifugo.
Habari Picha 11375
Naye Katibu wa Tawi la TUGHE katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Grace Mwaisyelage, amewahimiza wanawake kuendelea kuwaelimisha na kuwawezesha mabinti kwa kuwashirikisha katika shughuli za kiuchumi ili wawe viongozi na wafanyabiashara wakubwa siku zijazo.
Habari Picha 11376
Habari Picha 11377

You Might Also Like

TRAWU Yapigania Wafanyakazi TAZARA Nyongeza Ya Mshahara

Rais Samia Amwonya Mwigulu Dhidi Ya Vishawishi

NIDA Yapata Kibali Maalum Kurekebisha Taarifa Kwa Walioghushi Ili  Kujisajili

Serikali Kuwasilisha Bungeni Nyenzo Kuu Tatu Zitakazowezesha Utekelezaji Dira 2050

Watumishi Wa Magereza Manyara Wapatiwa Majiko Ya Gesi  

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Nyamhokya Atoa Wito kwa Wanawake Kusimama Imara Kiuchumi
Next Article Wataalamu wa Fedha SADC Wakutana Pretoria Kujadili Bajeti
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Nchimbi Ahimiza Ushirikiano wa Wizara Katika Uhifadhi wa Mazingira
Habari March 10, 2026
Mtaka, Ndunguru Wakubaliana Ujenzi wa Maabara ya Kimkakati Njombe
Habari March 10, 2026
Wataalamu wa Fedha SADC Wakutana Pretoria Kujadili Bajeti
Habari March 9, 2026
Nyamhokya Atoa Wito kwa Wanawake Kusimama Imara Kiuchumi
Habari March 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?