MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yaweka Utaratibu Biashara Pembezoni mwa Barabara
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yaweka Utaratibu Biashara Pembezoni mwa Barabara
Habari

Serikali Yaweka Utaratibu Biashara Pembezoni mwa Barabara

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Kilombelo, Abubakary Asenga ameiuliza Serikali ni utaratibu gani unaopaswa kufuatwa na wananchi wanaofanya biashara pembezoni mwa barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS,) hususan katika maeneo ya Mkambe, Kidatu na Mkula.
Katika swali la nyongeza, Mbunge huyo ametaka kujua ni lini wananchi ambao hawajalipwa fidia kupisha ujenzi wa barabara ya Ifakara–Kidatu watalipwa stahiki zao.
Aidha, amehoji ni lini taa za barabarani katika barabara hiyo zitafungwa.
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya, amesema kuwa kwa mujibu wa Marekebisho ya Kanuni za Matumizi ya Barabara za Mwaka 2025, Kanuni ya 36(4) imeweka utaratibu mahsusi kwa wafanyabiashara wanaotaka kutumia maeneo yaliyopo pembezoni mwa barabara.
Amefafanua kuwa mfanyabiashara anatakiwa kujaza fomu maalum ya maombi inayotolewa na TANROADS na kulipia ada ya maombi kabla ya kuwasilisha fomu hiyo.
Amesema baada ya kupokea maombi, TANROADS itayachakata na yale yatakayokidhi vigezo yatapatiwa kibali pamoja na kuarifiwa gharama zinazopaswa kulipwa kwa mujibu wa sheria.
Kuhusu fidia, Kasekenya amesema kuwa Kamati imeundwa chini ya Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wananchi ambao hawajalipwa au wamepata upungufu wa fidia, baada ya Serikali kujiridhisha kuwa wanastahili, wananchi hao watalipwa fidia zao.
Kuhusu taa za barabarani, alisema kuwa kuna taratibu zinazoendelea za uwekaji wa taa, na kwamba barabara zote mpya, ikiwemo Ifakara–Kidatu, zitawekewa taa za barabarani.

You Might Also Like

DART Toeni Fursa Kwa Watanzania Kuwekeza kwenye Mwendokasi -Mchengerwa

Wanafunzi Shule Ya Anlex, Walimu Wao Watinga Bungeni

Rafiki Mkubwa wa Trump, Elon Musk atanufaika vipi baada ya kumuunga mkono?  

Serikali Yaeleza Mikakati Ya Kuwezesha Vijana Katika Soko La Ajira

Mtaka, Ndunguru Wakubaliana Ujenzi wa Maabara ya Kimkakati Njombe

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TEHAMA Kuchochea Uchumi wa Kidijitali, Serikali Yatenga Sh Bil Tano Kwa Kampuni Changa
Next Article Makampuni 408 Ya Tanzania Yaruhusiwa Kusafirisha Mazao Ya Kilimo Kwenda China
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wananchi Washauriwa Kutumia  Wataalam Wa Ujenzi Kuepuka Madhara
Habari July 14, 2026
July 14, 2026
Uncategorized July 14, 2026
TANESCO Kutambulisha Mfumo Wa Kufunga Nyaya Kwenye Nyumba Ukifuatilia Matumizi Ya Umeme
Habari July 13, 2026
Wananchi Waendelea Kunufaika Na Ofa Za TTCL Sabasaba 2026
Habari July 13, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?