MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wizara  Ya Maliasili Na Utalii Ilivyotamba Na Historia Ya Faru John Na Faru Fausta Mbele Ya Kamati Ya Bunge
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wizara  Ya Maliasili Na Utalii Ilivyotamba Na Historia Ya Faru John Na Faru Fausta Mbele Ya Kamati Ya Bunge
Habari

Wizara  Ya Maliasili Na Utalii Ilivyotamba Na Historia Ya Faru John Na Faru Fausta Mbele Ya Kamati Ya Bunge

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi wetu, Dodoma.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt.Ashatu Kijaji  ameendelea kuongoza menejimenti ya wizara hiyo mbele ya kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuelezea kazi,majukumu ,muundo na changamoto za wizara hiyo na taasisi zake.

Katika mawasilisho mbalimbali yaliyofanyika mbele ya kamati hiyo kutoka kwa taasisi zilizoko chini ya wizara hiyo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiongozwa na Kamishna wa uhifadhi  Bw. Abdulrazaq Badru iliwasilisha  taarifa yake ikiwa na mafanikio makubwa katika uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.

Katika kikao hicho Ngorongoro iliwakumbusha  wabunge kuhusiana na historia isiyofutika ya faru wakubwa wawili ambao waliishi katika hifadhi hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Habari Picha 10888

Amesema Faru hao ni Fausta aliyezaliwa mwaka 1965 na kufa mwaka 2019  na faru John aliyezaliwa mwaka 1978 na kufa mwaka 2016.

Amesema Ngorongoro imewaweka kwenye historia  faru hao ili kuwaonesha watanzania umuhimu wa kuhifadhi  faru ambapo idadi yake ndani ya hifadhi hiyo inazidi kuongezeka  na kuvutia  watalii kutoka ndani na nje  ya nchi na hivyo kuwa na mchango mkubwa katika uingizaji wa fedha za kigeni.

Amesema Faru John  ndani ya hifadhi ya Ngorongoro  alijulikana pia  kama Bingwa wa mapenzi ama dume la mbegu kutokana na kuweza kuizunguka hifadhi yote akitafuta faru  majike  ili aweze kushiriki nao tendo la ndoa huku upendo wake ukitawaliwa na wivu wa kupindukia.

Amesema tabia nyingine ya faru  huyo   ilikuwa ni  utawala wa muda mrefu ndani ya hifadhi  hivyo alikuwa  chanzo kikubwa cha migogoro na kutaka kila faru jike awe naye peke yake hali ambayo mwaka 2011 alimuua faru  CHAUSI  kwa kugombea jike hii inadhihirisha ni jinsi gani mapenzi yanaua.

Ameongeza  kuwa tofauti na faru John, Faru Fausta, ndiye  faru pekee aliyeweza kuishi ndani ya hifadhi  ya Ngorongoro kwa muda mrefu wa miaka 54 na inasemekana pia amevunja rekodi  ya kidunia kuwa miongoni mwa faru wachache weusi walioweza   kuishi miaka mingi.

“Faru  Fausta licha ya kupandwa na madume mbalimbali ikiwemo faru John, hakubahatika kupata mtoto na kwa  mujibu wa wataalam wa wanyama  haikubainika ni kwanini faru Fausta katika umri wake wote wa miaka 54 hakujaaliwa  uzazi,” amesema.

Amesema Kisayansi faru anaweza asipate mtoto kutokana na kuwa na matatizo katika mfumo wa uzazi  ikiwa ni pamoja na kuchelewa kupata mimba ambapo faru akiwa na hali hiyo katika  umri unaotakiwa  anakuwa na homoni kiasi kidogo za jike na hivyo kushindwa kupata mimba.

“Wataalam wanasema kuwa Faru Fausta inawezekana aliishi muda mrefu kwa sababu hakuwa na msongo wa mawazo wa  kushika mimba,kulea watoto wala kunyonyesha zaidi ya kula bata na kushiriki mapenzi na faru wenzake,” amesema.

You Might Also Like

Miradi Ufungaji Mifumo Ya Umeme Jua 20,000 Mbioni Kuanza

Hospitali ya Temeke kufanyiwa maboresho eneo la huduma Kwa wateja

BRELA kuanza kuwasajili wakulima

Rais Samia Awatega Wateule Wake

Mgombea Urais NCCR-Mageuzi Atoa Wito kwa Wananchi Kujitokeza Kupiga Kura

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Luswetula Aagiza Udhibiti Mkali wa Mikopo Kandamizi
Next Article Tume  Ya Ulinzi  Wa Taarifa Binafsi Yaongeza Muda Wa Taasisi Kujisajili
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?