Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 7, 2026
Habari Lucy Ngowi 20

Stamico Yahimiza Ubunifu, Uaminifu Na Kujituma

Mkurugenzi Mtendaji atoa ahadi kwa wafanyakazi, wachimbaji wadogo
Na Lucy Ngowi
GEITA: MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Venancy Mwase, amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kuendelea kuwa wabunifu, waaminifu na kujituma zaidi katika majukumu yao, huku akiahidi kuwashika mkono kwa karibu kutokana na juhudi na mafanikio wanayoendelea kuonyesha.
Amezungumza hayo  Septemba 28, 2025, wakati wa kufunga Maonesho ya Nane ya Sekta ya Madini yaliyofanyika Geita.
Habari Picha 9702
Amewapongeza wafanyakazi wa STAMICO kwa kazi nzuri wanayoifanya akisema,”Kushukuru ni jambo jema, lakini niwaambie  mnafanya kazi nzuri sana,”.
Ameahidi kuwasaidia wachimbaji wadogo hususani wanawake kwa kugawa pampu za maji kwa kusema,
“Nimeahidi mwenyewe. Kamilisheni utafiti wa mahitaji, tutaanza kutoa kwa awamu hadi akina mama wote waondokane na changamoto hiyo.”
Habari Picha 9705
Amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kuwawezesha wachimbaji wadogo wazawa hasa wanawake na vijana kupitia vifaa, elimu na miundombinu muhimu.
Pia amesema agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kutenga mashine inayotumika kwa ajili ya utafiti au uchimbaji wa madini (rig), moja mahsusi kwa wanawake tayari limeanza kutekelezwa, vifaa vikiwa karibu kukamilika.
Habari Picha 9706
“Tunafuata utaratibu ule ule: Crasha iko, shed iko, na sasa tunatafuta vijana wa kusaidia vikundi hatua kwa hatua,” amesema.
Mwase amesena STAMICO inaendelea kujipanga kuhakikisha inaongeza msaada mkubwa kwa wafanyakazi na wadau wa sekta ya madini.
“Kila kidogo Serikali inachotoa kupitia STAMICO, mafanikio yake yanaonekana. Kwa nini msipewe kikubwa? Hatujawahi kuangushwa.” amesema.
Habari Picha 9704
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA), Salma Ernest ametoa shukranikwa Mkurugenzi wa STAMICO kwa kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Malika wa Madini mkoani Geita.
Mradi uliowezesha wanawake kufanyika kwa tafiti za kijiolojia, kuundwa kwa vikundi vipya vya wanawake wachimbaji, Kutoa elimu kwa zaidi ya wanawake 640, Kugawa jokarasha tano kati ya 20 zilizopo nchini, na kusaidia ushiriki wa wanawake kwenye maonyesho ya mwaka huu 2025.
“Tumetembelea mabanda yote, tumetambulika sisi ni nani na tunafanya nini. Tumekutana na mabenki na makampuni makubwa  haya yote yametokea kwa sababu umetufungulia njia,” amesema.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.