MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ndejembi Akabidhiwa Ofisi Na Dkt. Biteko Aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu Na Waziri Wa Nishati
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ndejembi Akabidhiwa Ofisi Na Dkt. Biteko Aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu Na Waziri Wa Nishati
Habari

Ndejembi Akabidhiwa Ofisi Na Dkt. Biteko Aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu Na Waziri Wa Nishati

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
DODOMA: WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, ameahidi kuendeleza kazi na mafanikio yote yaliyofikiwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko, ili kuhakikisha azma na maono ya Serikali katika kufanikisha miradi ya kimkakati ifikapo mwaka 2030 yanatimia.
Ndejembi ametoa kauli hiyo leo, Novemba 20, 2025, wakati akipokea rasmi ofisi kutoka kwa Dkt. Biteko katika makao makuu ya Wizara ya Nishati yaliyopo Mtumba, jijini Dodoma.
Ameshukuru  kazi kubwa na utendaji uliotukuka wa Dkt. Biteko katika kipindi chote cha uongozi wake.
Habari Picha 10376
Amesema kuwa kipindi cha uongozi wa Dkt. Biteko kimeleta mageuzi makubwa katika sekta ya nishati, hususan katika kuboresha huduma, kuongeza ufanisi na kuimarisha tija katika ukuaji wa sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Kwa upande wake, Dkt. Biteko amempongeza Waziri Ndejembi kwa kuteuliwa kuongoza Wizara ya Nishati na kumuahidi ushirikiano wa karibu wakati wowote utakapohitajika ili kufanikisha maono makubwa ya Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta hiyo.
“Mengi niliyojifunza nikiwa Wizara ya Nishati yamenijenga, lakini kubwa zaidi ni sala zangu kwenu katika kutekeleza majukumu yenu ya kila siku,” amesema Biteko.
Hafla ya makabidhiano hayo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Felchesmi Mramba, pamoja na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati.

You Might Also Like

TPHPA yaonyesha ufanisi mkubwa udhibiti wa panya, kwelea kwelea

Silinde: Serikali bega kwa bega na wadau wa kilimo

VETA Yatahadharisha Changamoto ya Kuzidisha Uchanganyaji wa Chakula Cha Mifugo

Johari Ataka Ufasili wa Sheria za Uchaguzi Ukamilike

LATRA CCC Yatoa Angalizo Uhitaji Mkubwa Wa Wasafiri Mwisho Wa Mwaka

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Jamii Yaaswa Kujenga Utamaduni wa Kusoma Vitabu
Next Article Viongozi Wa Dini Zote Wajifungie Kuomba,Kujadili Na Kutoa Mapendekezo-SAU
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?