MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Vijana Wahimizwa Kuweka Akiba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Vijana Wahimizwa Kuweka Akiba
Habari

Vijana Wahimizwa Kuweka Akiba

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), CPA Beng’i Issa amewataka vijana kuweka akiba na kuacha tabia ya kutumia zaidi ya wanachokipata.

Beng’i ametoa rai hiyo  Dar es Salaam, wakati akizindua Taasisi ya Chase Your Dreams, inayolenga kuwa mkono wa matumaini kwa vijana wa Kitanzania wanaopambana kufikia ndoto zao katika uchumi, elimu na ujasiriamali.

Amesema iwapo vijana wakizingatia uwekaji akiba na  kutokutumia zaidi ya wanachopata, ni wazi kuwa watafanikiwa katika mipango yao, hivyo kutimiza ndoto zao.

“Ukipata elfu kumi, tumia elfu tano, Usitumie kupita kipato unachopata, la sivyo utakopa kwa ajili ya matumizi, wakati mikopo ni kwa ajili ya kuendeleza biashara ama uwekezaji”.

Katibu huyo amesema ujio wa Taasisi ya Chase unaleta hamasa mpya ya maendeleo ya vijana, hivyo ni imani yake baada ya miaka mitano kundi kubwa la vijana litakuwa limefikiwa.

Beng’i  amesema Taifa la Tanzania linaweza kupiga hatua kubwa kupitia kundi la vijana, hivyo ofisi yake itaweka kipaumbele kwenye kundi hilo.

“Maendeleo ya taifa yanategemea vijana. Serikali iko tayari kushirikiana na taasisi kama hizi, ili kuhakikisha vijana wanatimiza malengo yao na kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.”amesema.

Amesema mafanikio hayaji kwa bahati, bali kwa mpango, bidii na utekelezaji wa kile kinachowashinikiza ndani ya ndoto zao.

Kwa upande mwingine Beng’i amewataka vijana kujishughulisha na kuacha kukaa bure, kwani serikali imedhamiria kuwawezesha vijana, ikiwemo mpango wa kuanzishwa kwa Wizara ya Vijana, kama ilivyotajwa katika hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassani wakati akifungua Bunge la 13.

Amewataka vijana wasiiogope dunia ya mafanikio, akiweka bayana kuwa maisha kuna kushindwa na kusonga mbele, hivyo wakifeli wainuke na wasiogope kufanya mambo makubwa.

Amefafanua kuwa uchumi ni nguzo muhimu katika heshima ya mtu kwenye jamii hata familia, kwa kuwa kukosa fedha huweza kumdhalilisha mtu kwenye ndoa, familia au katika mazingira ya kijamii.

 

Habari Picha 10327

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Lightness Makondo, amesema Chase Your Dreams ilianzishwa kutokana na changamoto zinazowakabili vijana wa Kitanzania kwa kushindwa kufikia ndoto kutokana na ukosefu wa elimu sahihi, rasilimali na uongozi wa kitaaluma.

“Kila kijana ana ndoto ambayo inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika jamii. Ndoto isipotekelezwa inabaki kuwa maono yasiyo na dira,”amesema.

Mkurugenzi huyo amesema Chase ni mwanga mpya kwa vijana wa Kitanzania. “Ni mwaliko wa kuamka, kuchukua hatua, kuweka mipango na kutumia fursa zilizopo ili kujenga maisha bora, uchumi imara na taifa lenye nguvu ya vijana. Ndoto hazijengwi kwa maneno zinajengwa kwa vitendo, nidhamu, mipango, na ujasiri” amesema.

Naye Joanitha Jeremiah kutoka Visionary Youth Organization amesisitiza umuhimu wa vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa faida, ikiwemo kujifunza, kufanya biashara na kujenga mitandao ya maendeleo, badala ya kupoteza muda kwa malumbano, matusi na kuonyesha maisha ya kuigiza.

Wakili Fredric Usiku amewataka vijana kuacha woga kwani unachangia hasara kubwa sana. “Ukishindwa kufanya maamuzi, utashindwa kufika unapotaka,”amesema.

 

You Might Also Like

PSPTB Yatangaza Usajili wa Mitihani ya 31 ya Kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi

DC Atoa Wito kwa Tume ya Kurekebisha Sheria Kuzingatia Sheria Ndogondogo za Halmashauri

WCF Yaleta Utulivu Mahala Pa Kazi – Katambi

Silaa: Akili Mnemba, Roboti kuongeza ufanisi,ubunifu 

Mbinu Mpya za Kilimo kwa Vijana Zapata Umaarufu Nanenane Banda La VETA

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Samia Amwonya Mwigulu Dhidi Ya Vishawishi
Next Article Rais Samia Atangaza Baraza Jipya La Mawaziri
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?